2 Peter 3:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo wapenzi wangu, mkiwa mnaingojea siku ile, fanyeni bidii kuwa safi kabisa bila hatia mbele ya Mungu, na kuwa na amani naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu hii, wapendwa, kwa kuwa mnatazamia mambo haya, fanyeni bidii ili awakute bila mawaa wala dosari, na mkiwa na amani kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Rafiki wapendwa, tunasubiri hili litokee. Hivyo jitahidini kadri mnavyoweza msiwe na dhambi wala kosa. Jitahidini kuwa na amani na Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa hiyo wapenzi wangu, mkiwa mnangojea Siku ile, fanyeni bidii kuwa safi kabisa bila hatia mbele ya Mungu, na kuwa na amani naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo wapenzi wangu, mkiwa mnaingojea siku ile, fanyeni bidii kuwa safi kabisa bila hatia mbele ya Mungu, na kuwa na amani naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu hii, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia kwa furaha mambo haya, fanyeni bidii ili awakute katika amani, bila mawaa wala dosari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu hii, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo haya, fanyeni bidii ili awakute katika amani, bila mawaa wala dosari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo, wapenzi, mnapoyangojea mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane mkiwa na amani, bila doa wala dosari mbele yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo wapenzi wangu, mkiwa mnaingojea siku ile, fanyeni bidii kuwa safi kabisa bila hatia mbele ya Mungu, na kuwa na amani naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo, wapendwa, mkiyatazamia hayo jikazeni, mpate kuonekana kuwa wenye utengemano pasipo kilema wala pasipo doadoa!*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu hiyo, wapendwa wangu, mukiwa munangojea mambo yale, mufanye bidii apate kuwakuta safi bila kosa lolote na mukae na amani pamoja naye.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.