2 Peter 3:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hayo ndiyo asemayo katika barua zake zote anapozungumzia suala hilo. Yapo mambo kadhaa katika barua zake yaliyo magumu kuyaelewa, mambo ambayo watu wajinga, wasio na msimamo, huyapotosha kama wanavyopotosha sehemu nyingine za Maandiko Matakatifu. Hivyo wanasababisha maangamizi yao wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huandika vivyo hivyo katika nyaraka zake zote, akizungumzia ndani yake mambo haya. Katika nyaraka zake kuna mambo mengine ambayo ni vigumu kuyaelewa, ambayo watu wajinga na wasio thabiti huyapotosha, kama wanavyopotosha Maandiko mengine na kujiletea maangamizi yao wenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndivyo anavyosema katika barua zake zote anapoandika kuhusu mambo haya. Sehemu zingine katika barua zake ni ngumu kuzielewa, na kuna baadhi ya watu huzifafanua vibaya. Watu hawa ni wajinga na wasioaminika. Watu hawa hutoa pia maana potofu kwa Maandiko mengine. Lakini kwa kufanya hivi wanajiangamiza wao wenyewe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hayo ndiyo asemayo katika barua zake zote anapozungumzia suala hilo. Yapo mambo kadhaa katika barua zake yaliyo magumu kuyaelewa, mambo ambayo watu wajinga, wasio na msimamo, huyapotosha kama wanavyopotosha sehemu nyingine za Maandiko Matakatifu. Hivyo wanasababisha maangamizi yao wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hayo ndiyo asemayo katika barua zake zote anapozungumzia suala hilo. Yapo mambo kadhaa katika barua zake yaliyo magumu kuyaelewa, mambo ambayo watu wajinga, wasio na msimamo, huyapotosha kama wanavyopotosha sehemu nyingine za Maandiko Matakatifu. Hivyo wanasababisha maangamizi yao wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huandika vivyo hivyo katika nyaraka zake zote akizungumzia ndani yake mambo haya. Katika nyaraka zake kuna mambo mengine ambayo ni vigumu kuyaelewa, ambayo watu wajinga na wasio thabiti huyapotosha kwa maangamizi yao wenyewe, kama wapotoshavyo pia Maandiko mengine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huandika vivyo hivyo katika nyaraka zake zote, akizungumzia ndani yake mambo haya. Katika nyaraka zake kuna mambo mengine ambayo ni vigumu kuyaelewa, ambayo watu wajinga na wasio thabiti huyapotosha kwa maangamizi yao wenyewe, kama wapotoshavyo pia Maandiko mengine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akisema juu ya mambo haya kama afanyavyo katika barua zake zote pia, katika barua hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuyaelewa na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wapotoavyo Maandiko mengine, na kujiletea maangamizi wao wenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hayo ndiyo asemayo katika barua zake zote anapozungumzia suala hilo. Yapo mambo kadhaa katika barua zake yaliyo magumu kuyaelewa, mambo ambayo watu wajinga, wasio na msimamo, huyapotosha kama wanavyopotosha sehemu nyingine za Maandiko Matakatifu. Hivyo wanasababisha maangamizi yao wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, anavyoandika katika barua zote akiyasema mambo hayo; lakini mle baruani mwake yamo maneno mengine yaliyo magumu ya kuyajua maana. Nao wasiofundishwa vema nao wasiomtegemea Mungu vema huyapindua, kama wanavyoyapindua hata Maandiko mengine; ndivyo, wanavyojiangamiza wenyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni vile ndivyo alivyoandika katika barua zote alimosema ndani yao juu ya mambo yale. Lakini ndani ya barua zile kunakuwa mambo mengine magumu kuyasikia. Na watu wajinga na wasiokamilika wanageuzageuza maana yake sawa vile wanavyogeuza sehemu zingine za Maandiko Matakatifu. Kwa njia ile wanajiangamiza wenyewe.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa khabari za mambo hayo mumo humo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa upotevu wao wenyewe.