2 Samuel 1:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, nilikwenda karibu naye na kumuua, kwa sababu nilikuwa na uhakika kuwa akianguka chini, hataweza kuishi zaidi. Lakini taji iliyokuwa kichwani pake na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, vyote nimekuletea wewe, bwana wangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo nikamkaribia na kumuua, kwa sababu nilijua kwamba baada ya kuanguka hangeweza kupona. Nami nikachukua lile taji lililokuwa kichwani mwake na utepe uliokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, nikasimama karibu naye, nikamwua, kwa sababu nalijua hakika ya kuwa hawezi kupona baada ya kuanguka; kisha nikaitwaa ile taji iliyokuwa kichwani mwake, na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, nilikwenda karibu naye na kumuua, kwa sababu nilikuwa na uhakika kuwa akianguka chini, hataweza kuishi zaidi. Lakini taji iliyokuwa kichwani pake na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, vyote nimekuletea wewe, bwana wangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo nikamkaribia nikamwua, kwa sababu nilijua kwamba baada ya kuanguka hangeweza kupona. Nami nikachukua lile taji lililokuwa kichwani mwake na utepe uliokuwa mkononi mwake nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo nikamkaribia nikamuua, kwa sababu nilijua kwamba baada ya kuanguka hangeweza kupona. Nami nikachukua lile taji lililokuwa kichwani mwake na utepe uliokuwa mkononi mwake nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, nikasimama karibu naye, nikamwua, kwa sababu nilijua hakika ya kuwa hawezi kupona baada ya kuanguka; kisha nikalitwaa lile taji lililokuwa kichwani mwake, na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, nilikwenda karibu naye na kumuua, kwa sababu nilikuwa na uhakika kuwa akianguka chini, hataweza kuishi zaidi. Lakini taji iliyokuwa kichwani pake na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, vyote nimekuletea wewe, bwana wangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nilipokuja hapo, alipokuwa, nikamwua, kwani nilijua, ya kuwa hawezi kupona kwa hivyo, alivyoanguka;. kisha nikakichukua kilemba chake kichwani pake na kikuku chake mkononi pake, nimevileta hapa kwa bwana wangu, ni hivi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, nikasimama karibu naye, nikamwua, kwa sababu nalijua hakika ya kuwa hawezi kupona baada ya kuanguka; kisha nikaitwaa ile taji iliyokuwa kichwani mwake, na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, nilikwenda karibu naye na kumwua, kwa sababu nilikuwa na uhakika kwamba akianguka chini, hataweza kuishi zaidi. Lakini taji iliyokuwa juu ya kichwa chake na kikomo kilichokuwa kwenye mukono wake, vyote nimekuletea wewe, bwana wangu.”