2 Samuel 1:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akamwuliza yule kijana aliyempasha habari, “Unatoka wapi?” Yeye akajibu, “Mimi ni Mmaleki, lakini ninaishi katika nchi yako kama mgeni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akamwambia yule kijana aliyemletea taarifa, “Wewe unatoka wapi?” Akamjibu, “Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Watoka wapi wewe? Akajibu, Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akamwuliza yule kijana aliyempasha habari, “Unatoka wapi?” Yeye akajibu, “Mimi ni Mmaleki, lakini ninaishi katika nchi yako kama mgeni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akamwambia yule mwanaume kijana aliyemletea taarifa, “Wewe ni mwenyeji wa wapi?” Akamjibu, “Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akamwambia yule kijana aliyemletea taarifa, “Wewe ni mwenyeji wa wapi?” Akamjibu, “Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Unatoka wapi wewe? Akajibu, Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akamwuliza yule kijana aliyempasha habari, “Unatoka wapi?” Yeye akajibu, “Mimi ni Mmaleki, lakini ninaishi katika nchi yako kama mgeni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Dawidi akamwuliza huyo kijana aliympasha habari hizi: Wewe u mtu wa wapi? Akasema: Mimi ni mwana wa mtu mgeni wa Amaleki.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Watoka wapi wewe? Akajibu, Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akamwuliza yule kijana aliyemupasha habari: “Unatoka wapi?” Yeye akajibu: “Mimi ni Mwamaleki, lakini ninaishi katika inchi yako kama mugeni.”