2 Samuel 1:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule kijana akamjibu, “Kwa bahati, nilikuwapo mlimani Gilboa. Nilimwona Shauli ameegemea mkuki wake na magari ya wapandafarasi ya adui zake yalikuwa yanamsonga sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule kijana akasema, “Nilijipata huko Mlima Gilboa, naye Sauli alikuwa huko akiegemea mkuki wake, na magari ya vita na wapanda farasi wa upande wa adui wakawa wamemkaribia sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule kijana aliyempa habari akasema, Nalikuwapo kwa nasibu juu ya kilima cha Gilboa, na tazama, Sauli alikuwa ameegemea fumo lake; na tazama, magari na wapanda farasi wanamfuatia kwa kasi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule kijana akamjibu, “Kwa bahati, nilikuwapo mlimani Gilboa. Nilimwona Shauli ameegemea mkuki wake na magari ya wapandafarasi ya adui zake yalikuwa yanamsonga sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule kijana mwanaume akasema, “Ilitokea nikawa juu ya Mlima Gilboa, naye Sauli alikuwako huko akiwa ameegemea mkuki wake, na magari ya vita na wapanda farasi wa upande wa adui wakawa wamemkaribia sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule kijana akasema, “Nilijipata huko Mlima Gilboa, naye Sauli alikuwa huko akiegemea mkuki wake, na magari ya vita na wapanda farasi wa upande wa adui wakawa wamemkaribia sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yule kijana aliyempa habari akasema, Nilikuwapo kwa nasibu juu ya kilima cha Gilboa, na tazama, Sauli alikuwa ameegemea fumo lake; na tazama, magari na wapanda farasi wanamfuatia kwa kasi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule kijana akamjibu, “Kwa bahati, nilikuwapo mlimani Gilboa. Nilimwona Shauli ameegemea mkuki wake na magari ya wapandafarasi ya adui zake yalikuwa yanamsonga sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule kijana aliyempasha hizi habari akamwambia: Ikanitukia, nifike mlimani kwa Gilboa, mara nikamwona Sauli, akiuegemea mkuki wake, nayo magari pamoja na wapanda farasi wakamsonga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule kijana aliyempa habari akasema, Nalikuwapo kwa nasibu juu ya kilima cha Gilboa, na tazama, Sauli alikuwa ameegemea fumo lake; na tazama, magari na wapanda farasi wanamfuatia kwa kasi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule kijana akamujibu: “Kwa bahati, nilikuwa juu ya mulima Gilboa. Nilimwona Saulo akiegemea mukuki wake na magari ya waaskari wapanda-farasi ya waadui zake yalikuwa yanamusonga sana.