2 Samuel 10:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Waaramu walikimbia mbele ya Waisraeli. Daudi aliwaua Waaramu 700 waliokuwa madereva wa magari ya vita, wapandafarasi 40,000. Pia alimwumiza Shobaki kamanda wa jeshi lao, naye akafia papo hapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari ya vita mia saba na askari wao wa miguu elfu arobaini. Vilevile alimpiga Shobaki jemadari wa jeshi lao, naye akafa huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi arobaini elfu, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Waaramu walikimbia mbele ya Waisraeli. Daudi aliwaua Waaramu 700 waliokuwa madereva wa magari ya vita, wapandafarasi 40,000. Pia alimwumiza Shobaki kamanda wa jeshi lao, naye akafia papo hapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akaua watu wao mia saba wapanda magari yao ya vita na askari wao wa miguu 40,000. Vile vile alimpiga Shobaki jemadari wa jeshi lao, naye akafa huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari mia saba na askari wao wa miguu 40,000. Vilevile alimpiga Shobaki jemadari wa jeshi lao, naye akafa huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi elfu arobaini, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Waaramu walikimbia mbele ya Waisraeli. Daudi aliwaua Waaramu 700 waliokuwa madereva wa magari ya vita, wapandafarasi 40,000. Pia alimwumiza Shobaki kamanda wa jeshi lao, naye akafia papo hapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Washami wakawakimbia Waisiraeli, Dawidi akaua kwao Washami farasi waliovuta magari 700 na wapanda farasi 40000, hata Sobaki, mkuu wa vikosi vyao, akampiga, naye akafa papo hapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi arobaini elfu, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Waaramu walikimbia mbele ya Waisraeli. Daudi aliwaua Waaramu mia saba waliokuwa waendeshaji wa magari ya vita, waaskari wapanda-farasi elfu makumi ine. Vilevile alimwumiza Sobaki, jemadari wa waaskari wao, naye akakufia palepale.