2 Samuel 10:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wakuu wa Waamori walimwambia bwana wao, Hanuni, “Je, unadhani kwamba Daudi kwa kukutumia watu wa kukufariji anamheshimu baba yako? Je, Daudi hakuwatuma watu hawa kwako ili kuuchunguza na kuupeleleza mji halafu wauteke?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni bwana wao, “Unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kukutumia watu ili kuonesha masikitiko? Je, Daudi hakuwatuma watu hawa kuchunguza na kuupeleleza mji ili kuupindua?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia Hanuni, bwana wao, Je! Waona ya kuwa Daudi amemheshimu babayo kwa kutuma kwako wafariji? Je! Daudi hakuwapeleka watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, na kuupeleleza, na kuuangamiza?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wakuu wa Waamori walimwambia bwana wao, Hanuni, “Je, unadhani kwamba Daudi kwa kukutumia watu wa kukufariji anamheshimu baba yako? Je, Daudi hakuwatuma watu hawa kwako ili kuuchunguza na kuupeleleza mji halafu wauteke?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni bwana wao, “unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kukutumia watu ili kuonyesha masikitiko? Je, Daudi hakuwatuma watu hawa kuchunguza na kuupeleleza mji ili kuupindua?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni bwana wao, “unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kukutumia watu ili kuonyesha masikitiko? Je, Daudi hakuwatuma watu hawa kuchunguza na kuupeleleza mji ili kuupindua?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, bwana wao, Je! Waona ya kuwa Daudi amemheshimu babayo kwa kutuma kwako wafariji? Je! Daudi hakuwapeleka watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, na kuupeleleza, na kuuangamiza?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wakuu wa Waamori walimwambia bwana wao, Hanuni, “Je, unadhani kwamba Daudi kwa kukutumia watu wa kukufariji anamheshimu baba yako? Je, Daudi hakuwatuma watu hawa kwako ili kuuchunguza na kuupeleleza mji halafu wauteke?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia bwana wao Hanuni; Je? Dawidi anataka kweli kumheshimu baba yako machoni pako akituma kwako wajumbe wa kukutuliza moyo? Dawidi hakuwatuma watumishi wake kwako kuuchunguza mji huu na kuupeleleza, apate kuufudikiza?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia Hanuni, bwana wao, Je! Waona ya kuwa Daudi amemheshimu babayo kwa kutuma kwako wafariji? Je! Daudi hakuwapeleka watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, na kuupeleleza, na kuuangamiza?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wakubwa wa Waamori walimwambia bwana wao, Hanuni: “Unazani kwamba Daudi kwa kukutumia watu wa kukufariji anamuheshimu baba yako? Daudi hakuwatuma watu hawa kwako kwa kuuchunguza na kuupeleleza muji halafu wauteke?”