2 Samuel 10:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliona aibu mno kurudi nyumbani. Daudi alipopashwa habari alituma watu kuwalaki kwani hao wajumbe waliona aibu sana. Naye mfalme aliwaambia, “Kaeni mjini Yeriko, hata mtakapoota ndevu, kisha mrudi nyumbani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi alipoambiwa jambo hili, akatuma wajumbe ili kwenda kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko hadi ndevu zenu ziote, ndipo mje.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu walipomwambia Daudi habari hizo, akatuma watu kuwalaki; kwa sababu watu hao walikuwa wametahayarika sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hata mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliona aibu mno kurudi nyumbani. Daudi alipopashwa habari alituma watu kuwalaki kwani hao wajumbe waliona aibu sana. Naye mfalme aliwaambia, “Kaeni mjini Yeriko, hata mtakapoota ndevu, kisha mrudi nyumbani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi alipoambiwa jambo hili, akatuma wajumbe ili kwenda kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko mpaka ndevu zenu zikishakuwa ndipo mje.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi alipoambiwa jambo hili, akatuma wajumbe ili kwenda kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko mpaka ndevu zenu ziote ndipo mje.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu walipomwambia Daudi habari hizo, akatuma watu kuwalaki; kwa sababu watu hao walikuwa wameaibika sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hata mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliona aibu mno kurudi nyumbani. Daudi alipopashwa habari alituma watu kuwalaki kwani hao wajumbe waliona aibu sana. Naye mfalme aliwaambia, “Kaeni mjini Yeriko, hata mtakapoota ndevu, kisha mrudi nyumbani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu walipompasha Dawidi habari hizo, akatuma wengine kuwaendea njiani, kwa kuwa watu hawa walikuwa wametwezwa sana; mfalme akawaambia: Kaeni Yeriko, mpaka ndevu zenu zikue tena, kisha rudini!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu walipomwambia Daudi habari hizo, akatuma watu kuwalaki; kwa sababu watu hao walikuwa wametahayarika sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hata mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipata haya sana kurudia kwao. Daudi alipopashwa habari, alituma watu kwa kuwapokea maana wale wajumbe walipata haya sana. Naye mufalme aliwaambia: “Mukae katika muji wa Yeriko, hata mutakapoota ndevu, kisha murudi kwa nyumba.”