2 Samuel 10:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waamoni walipoona kuwa wamemchukiza Daudi, walikodi wanajeshi Waaramu 20,000 waendao kwa miguu, kutoka Beth-rehobu na Soba; wanajeshi 12,000, kutoka Tobu, na mfalme Maaka akiwa na wanajeshi 1,000.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, wakaajiri askari wa miguu elfu ishirini, Waaramu kutoka Beth-Rehobu na Soba, pia mfalme wa Maaka na watu elfu moja, na vilevile watu elfu kumi na mbili kutoka Tobu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, wana wa Amoni wakatuma na kuwaajiri Washami wa Bethrehobu, na Washami wa Soba, askari ishirini elfu, na mfalme wa Maaka mwenye watu elfu, na watu wa Tobu watu kumi na mbili elfu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waamoni walipoona kuwa wamemchukiza Daudi, walikodi wanajeshi Waaramu 20,000 waendao kwa miguu, kutoka Beth-rehobu na Soba; wanajeshi 12,000, kutoka Tobu, na mfalme Maaka akiwa na wanajeshi 1,000.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa harufu mbaya kwenye pua za Daudi, wakaajiri askari wa miguu 20,000 wa Kiaramu kutoka Beth-Rehobu na Soba, pia mfalme wa Maaka pamoja na watu 1,000, na vile vile watu 12,000 kutoka Tobu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, wakaajiri askari wa miguu 20,000 Waaramu kutoka Beth-Rehobu na Soba, pia mfalme wa Maaka pamoja na watu 1,000, na vilevile watu 12,000 kutoka Tobu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Waamoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Waamoni wakatuma na kuwaajiri Washami wa Bethrehobu, na Washami wa Soba, askari elfu ishirini, na mfalme wa Maaka mwenye watu elfu moja, na watu wa Tobu watu elfu kumi na mbili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waamoni walipoona kuwa wamemchukiza Daudi, walikodi wanajeshi Waaramu 20,000 waendao kwa miguu, kutoka Beth-rehobu na Soba; wanajeshi 12,000, kutoka Tobu, na mfalme Maaka akiwa na wanajeshi 1,000.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Amoni walipoona, ya kuwa wamejichukizisha kwake Dawidi, ndipo, wana wa Amoni walipotuma watu kuwakodisha Washami wa Beti-Rehobu na Washami wa Soba, ni askari waliokwenda kwa miguu 20000, tena mfalme wa Maka na watu 1000 na watu 12000 wa Tobu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, wana wa Amoni wakatuma na kuwaajiri Washami wa Bethrehobu, na Washami wa Soba, askari ishirini elfu, na mfalme wa Maaka mwenye watu elfu, na watu wa Tobu watu kumi na mbili elfu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waamoni walipoona kwamba wamemuchukiza Daudi, walijilipia waaskari wa miguu wa Waaramu elfu makumi mbili kutoka Beti-Rehobu na Zoba, waaskari elfu kumi na mbili kutoka Tobu, na mufalme Maka akiwa na waaskari elfu moja.