2 Samuel 10:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waamoni walitoka na kujipanga tayari kwa vita kwenye lango la mji wa Raba, mji wao mkuu; nao Waaramu kutoka Soba na Rehobu na watu kutoka Tobu na Maaka walijipanga nyikani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waamoni wakatoka wakajipanga wakiwa tayari kwa vita langoni la mji wao, wakati Waaramu wa Soba na wa Rehobu, na wanaume wa Tobu na Maaka walikuwa peke yao kwenye eneo la wazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wana wa Amoni wakatoka, wakapanga vita mahali pa kuingilia lango; na Washami wa Soba, na wa Rehobu, na watu wa Tobu, na wa Maaka, walikuwa peke yao uwandani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waamoni walitoka na kujipanga tayari kwa vita kwenye lango la mji wa Raba, mji wao mkuu; nao Waaramu kutoka Soba na Rehobu na watu kutoka Tobu na Maaka walijipanga nyikani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waamoni wakatoka wakajipanga kwenye vita penye ingilio la lango la mji wao, wakati Waaramu wa Soba, wa Rehobu, watu wa Tobu na Maaka walikuwa peke yao kwenye eneo la wazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waamoni wakatoka wakajipanga wakiwa tayari kwa vita langoni la mji wao, wakati Waaramu wa Soba, wa Rehobu, watu wa Tobu na Maaka walikuwa peke yao kwenye eneo la wazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waamoni wakatoka, wakapanga vita mahali pa kuingilia lango; na Washami wa Soba, na wa Rehobu, na watu wa Tobu, na wa Maaka, walikuwa peke yao uwandani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waamoni walitoka na kujipanga tayari kwa vita kwenye lango la mji wa Raba, mji wao mkuu; nao Waaramu kutoka Soba na Rehobu na watu kutoka Tobu na Maaka walijipanga nyikani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Amoni wakatoka, wakajipanga penye lango la mji, wapige vita, nao Washami wa Soba na wa Rehobu na watu wa Tobu na wa Maka wakawa peke yao shambani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wana wa Amoni wakatoka, wakapanga vita mahali pa kuingilia lango; na Washami wa Soba, na wa Rehobu, na watu wa Tobu, na wa Maaka, walikuwa peke yao uwandani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waamoni walitoka na kujipanga tayari kwa vita kwenye mulango wa muji wa Raba, muji wao mukubwa; nao Waaramu kutoka Zoba na Rehobu na watu kutoka Tobu na Maka walijipanga katika mbuga.