2 Samuel 11:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mjumbe akamwambia Daudi, “Adui zetu walituzidi nguvu, wakatoka nje ya miji na kutushambulia nyikani. Hata hivyo sisi tuliwarudisha mpaka kwenye lango la mji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mjumbe akamwambia Daudi, “Watu walituzidi nguvu wakatoka nje ya mji dhidi yetu kwenye eneo la wazi, lakini tuliwarudisha nyuma hadi ingilio la mji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule mjumbe akamwambia Daudi, Watu hao walitushinda, wakatutokea nje hata uwandani, tukashindana nao hata mahali pa kuingilia langoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mjumbe akamwambia Daudi, “Adui zetu walituzidi nguvu, wakatoka nje ya miji na kutushambulia nyikani. Hata hivyo sisi tuliwarudisha mpaka kwenye lango la mji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mjumbe akamwambia Daudi, “Watu walituzidi nguvu wakatoka nje ya mji dhidi yetu kwenye eneo la wazi, lakini tuliwarudisha nyuma mpaka kwenye ingilio la mji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mjumbe akamwambia Daudi, “Watu walituzidi nguvu wakatoka nje ya mji dhidi yetu kwenye eneo la wazi, lakini tuliwarudisha nyuma mpaka kwenye ingilio la mji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yule mjumbe akamwambia Daudi, Watu hao walitushinda, wakatutokea nje hata uwandani, tukashindana nao hadi mahali pa kuingilia langoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mjumbe akamwambia Daudi, “Adui zetu walituzidi nguvu, wakatoka nje ya miji na kutushambulia nyikani. Hata hivyo sisi tuliwarudisha mpaka kwenye lango la mji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyo mjumbe akamwambia Dawidi: Wale watu wakatutolea nguvu na kututokea kwetu porini, nasi tukawaendea hata hapo pa kuliingilia lango la mji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule mjumbe akamwambia Daudi, Watu hao walitushinda, wakatutokea nje hata uwandani, tukashindana nao hata mahali pa kuingilia langoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mujumbe akamwambia Daudi: “Waadui zetu walitushinda nguvu, wakatoka inje ya miji na kutushambulia katika mbuga. Hata hivyo sisi tuliwarudisha mpaka kwenye mulango wa muji.