2 Samuel 11:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Muda wa matanga ulipokwisha, Daudi aliagiza Bathsheba achukuliwe na kupelekwa nyumbani kwake. Bathsheba akawa mke wa Daudi, naye akamzalia Daudi mtoto wa kiume. Lakini jambo hilo alilofanya Daudi lilimchukiza Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya muda wa maombolezo kwisha, Daudi akatumana aletwe nyumbani mwake. Naye akawa mkewe, na akamzalia mwana. Lakini jambo alilofanya Daudi lilimchukiza Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa, akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe, akamzalia mwana. Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Muda wa matanga ulipokwisha, Daudi aliagiza Bathsheba achukuliwe na kupelekwa nyumbani kwake. Bathsheba akawa mke wa Daudi, naye akamzalia Daudi mtoto wa kiume. Lakini jambo hilo alilofanya Daudi lilimchukiza Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya muda wa maombolezo kwisha, Daudi akamtaka aletwe nyumbani kwake, naye akawa mkewe, na akamzalia mwana. Lakini jambo alilokuwa amefanya Daudi lilimchukiza BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya muda wa maombolezo kwisha, Daudi akamtaka aletwe nyumbani kwake, naye akawa mkewe, na akamzalia mwana. Lakini jambo alilokuwa amefanya Daudi lilimchukiza bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa, akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe, akamzalia mtoto wa kiume. Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Muda wa matanga ulipokwisha, Daudi aliagiza Bathsheba achukuliwe na kupelekwa nyumbani kwake. Bathsheba akawa mke wa Daudi, naye akamzalia Daudi mtoto wa kiume. Lakini jambo hilo alilofanya Daudi lilimchukiza Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku za matanga zilipopita, Dawidi akatuma kumchukua nyumbani mwake, akawa mkewe, akamzalia mwana. Lakini jambo hili, Dawidi alilolifanya, likawa baya machoni pake Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa, akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe, akamzalia mwana. Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muda wa kufunga kilio ulipokwisha, Daudi aliagiza wamulete Batiseba na kumupeleka katika nyumba yake. Batiseba akakuwa muke wa Daudi, naye akamuzalia Daudi mutoto mwanaume. Lakini jambo hilo Daudi alilofanya lilimuchukiza Yawe.