2 Samuel 12:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu Daudi akamfariji Bathsheba mkewe. Akalala naye, naye akapata mimba na kujifungua mtoto wa kiume, ambaye Daudi alimwita Solomoni. Mwenyezi-Mungu alimpenda mtoto huyo,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Daudi akamfariji Bathsheba mkewe; akaingia kwake akakutana naye kimwili. Akazaa mwana, wakamwita jina Sulemani. Mwenyezi Mungu alimpenda Sulemani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Daudi akamfariji Bath-sheba mkewe, akaingia kwake, akalala naye; naye akazaa mwana, akamwita jina lake Sulemani. Naye Bwana akampenda;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu Daudi akamfariji Bathsheba mkewe. Akalala naye, naye akapata mimba na kujifungua mtoto wa kiume, ambaye Daudi alimwita Solomoni. Mwenyezi-Mungu alimpenda mtoto huyo,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Daudi akamfariji Bathsheba mkewe, akaingia kwake akakutana naye kimwili. Akazaa mwana, wakamwita jina lake Solomoni. BWANA alimpenda Solomoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Daudi akamfariji Bathsheba mkewe, akaingia kwake akakutana naye kimwili. Akazaa mwana, wakamwita jina lake Sulemani. bwana alimpenda Sulemani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Daudi akamfariji Bathsheba mkewe, akaingia kwake, akalala naye; naye akazaa mwana, akamwita jina lake Sulemani. Naye BWANA akampenda;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu Daudi akamfariji Bathsheba mkewe. Akalala naye, naye akapata mimba na kujifungua mtoto wa kiume, ambaye Daudi alimwita Solomoni. Mwenyezi-Mungu alimpenda mtoto huyo,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akamtuliza moyo mkewe Bati-Seba, akaingia kwake, akalala naye, kisha akazaa mtoto mume, akamwita jina lake Salomo (Mtulivu), naye Bwana akampenda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Daudi akamfariji Bath-sheba mkewe, akaingia kwake, akalala naye; naye akazaa mwana, akamwita jina lake Sulemani. Naye BWANA akampenda;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Daudi akamufariji Batiseba muke wake. Akalala naye, naye akapata mimba na kuzaa mutoto mwanaume, naye Daudi alimwita Solomono. Yawe alimupenda mutoto yule,