2 Samuel 12:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja, yule tajiri alifikiwa na mgeni. Basi, tajiri huyo hakutaka kuchukua mmoja wa kondoo wake mwenyewe au ng'ombe wake, amchinjie mgeni wake, ila alikwenda na kumnyanganya yule maskini mwanakondoo wake, akamchinjia mgeni wake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Siku moja yule tajiri akafikiwa na mgeni, lakini huyo tajiri hakuchukua mmoja wa kondoo au ng’ombe wake mwenyewe amwandalie mgeni. Badala yake akachukua yule kondoo jike mdogo aliyekuwa mali ya yule maskini na kumwandalia yule mgeni wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata msafiri mmoja akamfikilia yule tajiri, naye akaacha kutwaa mmoja wa kondoo zake mwenyewe au mmoja wa ng'ombe zake mwenyewe, ili kumwandalia yule msafiri aliyemfikilia, bali alimnyang'anya yule maskini mwana-kondoo wake, akamwandalia yule mtu aliyemfikilia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja, yule tajiri alifikiwa na mgeni. Basi, tajiri huyo hakutaka kuchukua mmoja wa kondoo wake mwenyewe au ng'ombe wake, amchinjie mgeni wake, ila alikwenda na kumnyang'anya yule maskini mwanakondoo wake, akamchinjia mgeni wake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Siku moja yule tajiri akafikiwa na mgeni, lakini huyo tajiri akaacha kuchukua mmoja wa kondoo au ng'ombe wake mwenyewe amwandalie mgeni. Badala yake akachukua yule kondoo jike mdogo aliyekuwa mali ya yule maskini na kumwandalia yule mgeni wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Siku moja yule tajiri akafikiwa na mgeni, lakini huyo tajiri akaacha kuchukua mmoja wa kondoo au ng’ombe wake mwenyewe amwandalie mgeni. Badala yake akachukua yule kondoo jike mdogo aliyekuwa mali ya yule maskini na kumwandalia yule mgeni wake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha msafiri mmoja akamfikia yule tajiri, naye akaacha kutwaa mmoja wa kondoo zake mwenyewe au mmoja wa ng'ombe zake mwenyewe, ili kumwandalia yule msafiri aliyemfikia, bali alimnyang'anya yule maskini mwana-kondoo wake, akamwandalia yule mtu aliyemfikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja, yule tajiri alifikiwa na mgeni. Basi, tajiri huyo hakutaka kuchukua mmoja wa kondoo wake mwenyewe au ng'ombe wake, amchinjie mgeni wake, ila alikwenda na kumnyanganya yule maskini mwanakondoo wake, akamchinjia mgeni wake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku moja yule mkwasi akafikiwa na mgeni, akaona uchungu wa kuchukua kondoo wake au ng'ombe wake mmoja wa kumpa yule mpitaji aliyefikia kwake, basi, akakichukua kikondoo cha yule maskini, akamtengenezea yule mtu aliyefikia kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata msafiri mmoja akamfikilia yule tajiri, naye akaacha kutwaa mmoja wa kondoo zake mwenyewe au mmoja wa ng’ombe zake mwenyewe, ili kumwandalia yule msafiri aliyemfikilia, bali alimnyang’anya yule maskini mwana-kondoo wake, akamwandalia yule mtu aliyemfikilia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja, yule tajiri alifikiwa na mugeni. Basi, tajiri yule hakutaka kukamata kondoo mumoja kati ya kondoo wake mwenyewe au ngombe wake, amuchinjie mugeni wake, lakini alikwenda na kumunyanganya yule masikini mwana-kondoo wake, akamuchinjia mugeni wake.”