2 Samuel 12:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiwe huyo mtu! Sasa, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: ‘Mimi nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli na kukuokoa mikononi mwa Shauli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiwe huyo mtu! Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, nilikuokoa kutokana na mkono wa Sauli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Nathani akamwambia Daudi, Wewe ndiwe mtu huyo. Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nalikutia mafuta, uwe mfalme juu ya Israeli, nikakuokoa na mkono wa Sauli;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiwe huyo mtu! Sasa, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: ‘Mimi nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli na kukuokoa mikononi mwa Shauli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiwe huyo mtu! Hivi ndivyo asemavyo BWANA, Mungu wa Israeli: ‘Nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, nilikuokoa kutokana na mkono wa Sauli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiwe huyo mtu! Hivi ndivyo asemavyo bwana, Mungu wa Israeli: ‘Nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, nilikuokoa kutokana na mkono wa Sauli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Nathani akamwambia Daudi, Wewe ndiwe mtu huyo. BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nilikutia mafuta, uwe mfalme juu ya Israeli, nikakuokoa kutoka katika mkono wa Sauli;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiwe huyo mtu! Sasa, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: ‘Mimi nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli na kukuokoa mikononi mwa Shauli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Natani akamwambia Dawidi: Wewe ndiwe huyo mtu! Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Mimi nilikupaka mafuta, uwe mfalme wa Waisiraeli. Mimi nami nikakuponya mkononi mwa Sauli,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Nathani akamwambia Daudi, Wewe ndiwe mtu huyo. BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nalikutia mafuta, uwe mfalme juu ya Israeli, nikakuokoa na mkono wa Sauli;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Natani akamwambia Daudi: “Wewe ndiwe mutu yule! Sasa, Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: ‘Mimi nilikupakaa mafuta ukuwe mufalme juu ya Israeli. Nilikuokoa toka katika mikono ya Saulo.