2 Samuel 12:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa nini basi, umedharau neno langu mimi Mwenyezi-Mungu ukafanya uovu huu mbele yangu? Umemuua Uria Mhiti, kwa upanga, ukamchukua mke wake kuwa mkeo. Umewatumia Waamoni kumwua Uria vitani!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa nini ulilidharau neno la Mwenyezi Mungu kwa kufanya lililo ovu machoni pake? Ulimuua Uria Mhiti kwa upanga, na kumchukua mke wake awe mkeo. Ulimuua kwa upanga wa Waamoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa nini umelidharau neno la Bwana, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa wana wa Amoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa nini basi, umedharau neno langu mimi Mwenyezi-Mungu ukafanya uovu huu mbele yangu? Umemuua Uria Mhiti, kwa upanga, ukamchukua mke wake kuwa mkeo. Umewatumia Waamoni kumwua Uria vitani!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa nini ulilidharau neno la BWANA kwa kufanya lililo ovu machoni pake? Ulimwua Uria, Mhiti kwa upanga na kumchukua mke wake awe mkeo. Ulimwua kwa upanga wa Waamoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa nini ulilidharau neno la bwana kwa kufanya lililo ovu machoni pake? Ulimuua Uria, Mhiti kwa upanga na kumchukua mke wake awe mkeo. Ulimuua kwa upanga wa Waamoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa nini umelidharau neno la BWANA, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa Waamoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa nini basi, umedharau neno langu mimi Mwenyezi-Mungu ukafanya uovu huu mbele yangu? Umemuua Uria Mhiti, kwa upanga, ukamchukua mke wake kuwa mkeo. Umewatumia Waamoni kumwua Uria vitani!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu gani umelibeza neno la Bwana ukilifanya lililo baya machoni pake? Yule Mhiti Uria umemwua kwa upanga, ukamchukua mkewe, awe mke wako, ulipokwisha kumwua kwa panga za wana wa Amoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa nini umelidharau neno la BWANA, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa wana wa Amoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa nini basi, umezarau neno langu mimi Yawe na kufanya uovu huu mbele yangu? Umemwua Uria wa Hiti kwa upanga, ukamukamata muke wake kuwa muke wako. Umewatumia Waamoni kwa kumwua Uria katika vita!