2 Samuel 13:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Absalomu, alikuwa na dada yake mzuri aliyeitwa Tamari. Muda si muda, Amnoni, mtoto mwingine wa kiume wa Daudi, akampenda sana Tamari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikawa baada ya hayo, Amnoni mwana wa Daudi akampenda Tamari, dada yake Absalomu mwana wa Daudi, aliyekuwa mzuri wa sura.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Absalomu, alikuwa na dada yake mzuri aliyeitwa Tamari. Muda si muda, Amnoni, mtoto mwingine wa kiume wa Daudi, akampenda sana Tamari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikawa baada ya hayo, Amnoni mwana wa Daudi akampenda Tamari, umbu lake Absalomu mwana wa Daudi, ambaye alikuwa mzuri wa sura.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikawa baada ya hayo, Amnoni mwana wa Daudi akampenda Tamari, umbu lake Absalomu mwana wa Daudi, ambaye alikuwa mzuri wa sura.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na dada yake mzuri, aliyeitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Absalomu, alikuwa na dada yake mzuri aliyeitwa Tamari. Muda si muda, Amnoni, mtoto mwingine wa kiume wa Daudi, akampenda sana Tamari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo yalipokwisha kufanyika, Abisalomu, mwana wa Dawidi, alikuwa na umbu lake, jina lake Tamari, naye alikuwa mzuri; kwa hiyo Amunoni, mwana wa Dawidi, akampenda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Abusaloma mwana wa Daudi, alikuwa na dada yake muzuri sana aliyeitwa Tamari. Naye Amunoni, mwana mwingine wa Daudi, akamupenda sana Tamari.