2 Samuel 13:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Amnoni akamwambia Tamari, “Sasa niletee mikate hiyo chumbani kwangu, halafu unilishe.” Tamari aliichukua mikate aliyoiandaa na kuipeleka chumbani kwa kaka yake Amnoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Amnoni akamwambia Tamari, “Leta mkate hapa ndani ya chumba changu ili nipate kula kutoka mkononi mwako.” Basi Tamari akachukua mikate aliyoiandaa na kumletea Amnoni ndugu yake ndani ya chumba chake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Amnoni akamwambia Tamari, “Sasa niletee mikate hiyo chumbani kwangu, halafu unilishe.” Tamari aliichukua mikate aliyoiandaa na kuipeleka chumbani kwa kaka yake Amnoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Amnoni akamwambia Tamari, “Leta mkate hapa ndani ya chumba changu ili nipate kula kutoka mkononi mwako.” Basi Tamari akachukua mikate aliyoiandaa na kumletea Amnoni ndugu yake ndani ya chumba chake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Amnoni akamwambia Tamari, “Leta mkate hapa ndani ya chumba changu ili nipate kula kutoka mkononi mwako.” Basi Tamari akachukua mikate aliyoiandaa na kumletea Amnoni ndugu yake ndani ya chumba chake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoiandaa, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Amnoni akamwambia Tamari, “Sasa niletee mikate hiyo chumbani kwangu, halafu unilishe.” Tamari aliichukua mikate aliyoiandaa na kuipeleka chumbani kwa kaka yake Amnoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Amunoni akamwambia Tamari: Kilete hicho chakula chumbani humu, nikile na kukipokea mkononi mwako! Tamari akavichukua hivyo vikate, alivyovitengeneza, akampelekea umbu lake Amunoni mle chumbani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Amunoni akamwambia Tamari: “Sasa uniletee mikate ile ndani ya chumba changu, halafu unikulishe.” Tamari alitwaa mikate aliyoitayarisha na kuipeleka ndani ya chumba cha kaka yake Amunoni.