2 Samuel 13:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Amnoni na yule kijana wakamtoa nje na kuufunga mlango kwa komeo. Tamari alikuwa amevaa vazi refu lenye mikono mirefu kwani hivyo ndivyo walivyovaa mabikira wa mfalme zamani hizo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, mtumishi wake akamtoa nje na kufunga mlango nyuma yake. Tamari alikuwa amevaa joho lililopambwa vizuri, kwa maana lilikuwa aina ya mavazi yaliyovaliwa na binti za mfalme waliokuwa mabikira.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamleta nje, akafunga mlango nyuma yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Amnoni na yule kijana wakamtoa nje na kuufunga mlango kwa komeo. Tamari alikuwa amevaa vazi refu lenye mikono mirefu kwani hivyo ndivyo walivyovaa mabikira wa mfalme zamani hizo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, mtumishi wake akamtoa nje na kufunga mlango nyuma yake. Tamari alikuwa amevaa joho lililopambwa vizuri, kwa maana lilikuwa ndilo aina ya vazi lililovaliwa na binti za kifalme walio mabikira.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, mtumishi wake akamtoa nje na kufunga mlango nyuma yake. Tamari alikuwa amevaa joho lililopambwa vizuri, kwa maana lilikuwa aina ya mavazi yaliyovaliwa na binti za mfalme waliokuwa mabikira.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamtoa nje, akafunga mlango nyuma yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Amnoni na yule kijana wakamtoa nje na kuufunga mlango kwa komeo. Tamari alikuwa amevaa vazi refu lenye mikono mirefu kwani hivyo ndivyo walivyovaa mabikira wa mfalme zamani hizo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alikuwa amevaa rinda refu la nguo za rangi, kwani ndiyo mavazi, watoto wa kike wa mfalme waliyoyavaa siku za kuwa wanawali. Yule mtumishi wake alipomtoa nje na kufunga mlango, alipokwisha kutoka,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamleta nje, akafunga mlango nyuma yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Amunoni na yule kijana wakamutosha inje na kufunga mulango kwa kifungio. Tamari alikuwa amevaa kanzu ndefu yenye mikono mirefu maana hivi ndivyo mabikira wa mufalme walivyovaa zamani.