2 Samuel 13:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Amnoni aliteseka sana hata akajifanya mgonjwa kwa sababu ya dada yake Tamari hasa kwa vile Tamari alikuwa bikira, na ilionekana jambo lisilowezekana kwa Amnoni kufanya chochote naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amnoni akasumbuka sana kuhusu Tamari hata akaugua, kwa kuwa Tamari alikuwa bikira, na ilionekana kwamba haiwezekani Amnoni kumfanyia jambo lolote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya umbu lake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni vigumu kumtendea neno lo lote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Amnoni aliteseka sana hata akajifanya mgonjwa kwa sababu ya dada yake Tamari hasa kwa vile Tamari alikuwa bikira, na ilionekana jambo lisilowezekana kwa Amnoni kufanya chochote naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amnoni akasumbuka sana kuhusu Tamari hata akaugua, kwa kuwa Tamari alikuwa bikira, na ilionekana kwamba haiwezekani Amnoni kumfanyia jambo lo lote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amnoni akasumbuka sana kuhusu Tamari hata akaugua, kwa kuwa Tamari alikuwa bikira, na ilionekana kwamba haiwezekani Amnoni kumfanyia jambo lolote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya yule dada yake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni vigumu kumtendea neno lolote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Amnoni aliteseka sana hata akajifanya mgonjwa kwa sababu ya dada yake Tamari hasa kwa vile Tamari alikuwa bikira, na ilionekana jambo lisilowezekana kwa Amnoni kufanya chochote naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Amunoni akasongeka moyoni, akapata kuwa mgonjwa kwa ajili ya umbu lake Tamari, kwani alikuwa mwanamwali, naye Amunoni akaviona kuwa vigumu sana kumfanyizia lo lote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya umbu lake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni vigumu kumtendea neno lo lote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Amunoni aliteseka sana hata akajifanya mugonjwa kwa sababu ya dada yake Tamari kufuatana na vile Tamari alikuwa angali bikira, na ilionekana jambo lisilowezekana kwa Amunoni kufanya kitu chochote naye.