2 Samuel 13:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Absalomu akawaambia watumishi wake, “Mwangalieni Amnoni atakapokuwa amekunywa divai na kufurahi. Nitakapowaambia, ‘Mpigeni Amnoni,’ muueni. Hiyo ni amri yangu kwenu. Jipeni moyo na muwe hodari.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Absalomu aliagiza watu wake, “Sikilizeni! Amnoni atakapokuwa amekunywa mvinyo na kulewa sana nami nikiwaambia, ‘Mpigeni Amnoni,’ basi muueni. Msiogope. Je, si mimi niliyewapa amri hii? Kuweni hodari na wenye ushujaa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, ndipo mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, iweni na ujasiri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Absalomu akawaambia watumishi wake, “Mwangalieni Amnoni atakapokuwa amekunywa divai na kufurahi. Nitakapowaambia, ‘Mpigeni Amnoni,’ muueni. Hiyo ni amri yangu kwenu. Jipeni moyo na muwe hodari.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Absalomu aliagiza watu wake, “Sikilizeni! Wakati Amnoni atakapokuwa amekunywa mvinyo na kulewa sana nami nikiwaambia, ‘Mpigeni Amnoni,’ basi mwueni. Msiogope. Je, si mimi niliyewapa amri hii? Iweni hodari na wenye ushujaa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Absalomu aliagiza watu wake, “Sikilizeni! Wakati Amnoni atakapokuwa amekunywa mvinyo na kulewa sana nami nikiwaambia, ‘Mpigeni Amnoni,’ basi muueni. Msiogope. Je, si mimi niliyewapa amri hii? Kuweni hodari na wenye ushujaa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, kisha mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, na wenye ujasiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Absalomu akawaambia watumishi wake, “Mwangalieni Amnoni atakapokuwa amekunywa divai na kufurahi. Nitakapowaambia, ‘Mpigeni Amnoni,’ muueni. Hiyo ni amri yangu kwenu. Jipeni moyo na muwe hodari.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Abisalomu akawaagiza vijana wake kwamba: Angalieni! Moyo wa Amunoni utakapochangamka kwa kunywa mvinyo, nitawaambieni: Mpigeni Amunoni! Ndipo, mtakapomwua pasipo kuogopa. Kwani ni mimi ninayewaagiza ninyi kuvifanya. Jipeni mioyo, mpate kuwa wenye nguvu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, ndipo mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, iweni na ujasiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Abusaloma akawaambia watumishi wake: “Mumwangalie Amunoni atakapokuwa amekunywa divai na kufurahi. Nitakapowaambia: ‘Mumupige Amunoni’, mumwue. Hiyo ni amri yangu kwenu. Mujipe moyo na mukuwe hodari.”