2 Samuel 13:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yonadabu akamwambia, “Wewe jilaze kitandani ukidai kuwa u mgonjwa. Baba yako atakapokuja kukuona, wewe msihi ukisema, ‘Mruhusu dada yangu, Tamari, aje aniletee mkate nipate kula na aniandalie chakula mbele yangu ili nikione naye mwenyewe anilishe.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yonadabu akamwambia, “Nenda ukalale kitandani na ujifanye kuwa mgonjwa. Baba yako atakapokuja kukuona mwambie, ‘Ningependa Tamari dada yangu aje kunipatia chochote ili nile. Tafadhali mruhusu aje na kuniandalia chakula mbele yangu ningali ninamwona, ili nipate kula kutoka mkononi mwake.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile mkononi mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yonadabu akamwambia, “Wewe jilaze kitandani ukidai kuwa u mgonjwa. Baba yako atakapokuja kukuona, wewe msihi ukisema, ‘Mruhusu dada yangu, Tamari, aje aniletee mkate nipate kula na aniandalie chakula mbele yangu ili nikione naye mwenyewe anilishe.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yonadabu akamwambia, “Nenda ukalale kitandani na ujifanye kuwa mgonjwa. Baba yako atakapokuja kukuona mwambie, ‘Ningependa Tamari dada yangu aje kunipatia cho chote ili nile. Tafadhali mruhusu aje na kuniandalia chakula mbele yangu ningali ninamwona, ili nipate kula kutoka mkononi mwake.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yonadabu akamwambia, “Nenda ukalale kitandani na ujifanye kuwa mgonjwa. Baba yako atakapokuja kukuona mwambie, ‘Ningependa Tamari dada yangu aje kunipatia chochote ili nile. Tafadhali mruhusu aje na kuniandalia chakula mbele yangu ningali ninamwona, ili nipate kula kutoka mkononi mwake.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile mkononi mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yonadabu akamwambia, “Wewe jilaze kitandani ukidai kuwa u mgonjwa. Baba yako atakapokuja kukuona, wewe msihi ukisema, ‘Mruhusu dada yangu, Tamari, aje aniletee mkate nipate kula na aniandalie chakula mbele yangu ili nikione naye mwenyewe anilishe.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yonadabu akamwambia: Lala kitandani pako kuwa kama mgonjwa sana! Kisha baba yako akija kukutazama, umwambie: Kama umbu langu Tamari angekuja kuniandalia chakula na kukitengeneza hicho chakula machoni pangu, nipate kuviona, basi, ningekula na kuvipokea mkononi mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile mkononi mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yonadabu akamwambia: “Wewe ujilalishe katika kitanda na ujifanye kuwa mugonjwa. Baba yako atakapokuja kukuona, wewe umusihi ukisema: ‘Umuruhusu dada yangu, Tamari, akuje aniletee mukate nipate kula na anitayarishie chakula mbele yangu kusudi nikione naye mwenyewe anikulishe.’ ”