2 Samuel 14:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mwanamke akamwambia, “Tafadhali, mfalme, niombee kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ili yule ndugu yangu ambaye angelipiza kisasi cha mauaji ya mwanangu asifanye hatia nyingine kubwa ya kumwua yule mtoto wangu mwingine.” Mfalme Daudi akamwambia, “Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo, hakuna hata unywele mmoja wa mwanao utakaoanguka chini.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyo mwanamke akasema, “Basi mfalme na amwombe Mwenyezi Mungu, Mungu wake, ili kuzuia mlipiza kisasi cha damu kuongeza juu ya uharibifu, ili mwanangu asije akaangamizwa.” Mfalme akasema, “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, hakuna unywele mmoja wa kichwa cha mwanao utakaoanguka chini.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akajibu, Nakusihi, mfalme na amkumbuke Bwana, Mungu wako, ili mlipiza kisasi cha damu asizidi kuharibu, wasije kumharibu mwanangu. Naye akasema, Aishivyo Bwana, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa mwanao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mwanamke akamwambia, “Tafadhali, mfalme, niombee kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ili yule ndugu yangu ambaye angelipiza kisasi cha mauaji ya mwanangu asifanye hatia nyingine kubwa ya kumwua yule mtoto wangu mwingine.” Mfalme Daudi akamwambia, “Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo, hakuna hata unywele mmoja wa mwanao utakaoanguka chini.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyo mwanamke akasema, “Basi mfalme na amwombe BWANA Mungu wake ili kuzuia mlipiza kisasi cha damu kuongeza juu ya uharibifu, ili kwamba mwanangu asije akaangamizwa.” Mfalme akasema, “Hakika kama aishivyo BWANA, hakuna unywele mmoja wa kichwa cha mwanao utakaoanguka chini.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyo mwanamke akasema, “Basi mfalme na amwombe bwana Mwenyezi Mungu wake ili kuzuia mlipiza kisasi cha damu kuongeza juu ya uharibifu, ili kwamba mwanangu asije akaangamizwa.” Mfalme akasema, “Hakika kama aishivyo bwana, hakuna unywele mmoja wa kichwa cha mwanao utakaoanguka chini.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akajibu, Nakusihi, mfalme na amkumbuke BWANA, Mungu wako, ili mlipiza kisasi cha damu asizidi kuharibu, wasije kumharibu mwanangu. Naye akasema, Aishivyo BWANA, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa mwanao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mwanamke akamwambia, “Tafadhali, mfalme, niombee kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ili yule ndugu yangu ambaye angelipiza kisasi cha mauaji ya mwanangu asifanye hatia nyingine kubwa ya kumwua yule mtoto wangu mwingine.” Mfalme Daudi akamwambia, “Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo, hakuna hata unywele mmoja wa mwanao utakaoanguka chini.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akajibu: Mfalme, mkumbuke Bwana Mungu wako, mwenye kulipiza damu asizidi kufanya mabaya, wakimwangamiza mwanangu. Akasema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, unywele mmoja tu wa mwanao hautaanguka chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akajibu, Nakusihi, mfalme na amkumbuke BWANA, Mungu wako, ili mlipiza kisasi cha damu asizidi kuharibu, wasije kumharibu mwanangu. Naye akasema, Aishivyo BWANA, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa mwanao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mwanamuke akamwambia: “Tafazali, mufalme, uniombee kwa Yawe, Mungu wako, kusudi yule ndugu yangu ambaye angelipiza kisasi kutokana na mauaji ya mwana wangu hatafanya kosa lingine kubwa la kumwua yule mutoto wangu mwingine.” Mufalme Daudi akamwambia: “Kama vile Yawe anavyoishi, hakuna hata unywele mumoja wa mwana wako utakaoanguka chini.”