2 Samuel 14:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme akamwuliza, “Je, Yoabu anahusika katika jambo hili?” Yule mwanamke akasema, “Kama uishivyo, bwana wangu mfalme, mtu hawezi kukwepa kulia au kushoto kuhusu jambo ulilosema bwana wangu mfalme. Yoabu yule mtumishi wako ndiye aliyenituma. Ni yeye aliyeniambia maneno yote haya niliyokuambia mimi mtumishi wako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akauliza, “Je, mkono wa Yoabu haupo pamoja nawe katika jambo hilo lote?” Huyo mwanamke akajibu, “Hakika kama uishivyo, bwana wangu mfalme, hakuna yeyote anayeweza kugeuka kulia wala kushoto kutokana na chochote anachosema bwana wangu mfalme. Naam, ni mtumishi wako Yoabu ndiye alinifundisha kufanya hivi, naye ndiye aliweka maneno haya yote kinywani mwa mtumishi wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akasema, Je! Si mkono wa Yoabu ulio pamoja nawe katika haya yote? Mwanamke akajibu, akasema, Kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mfalme, hapana mtu awezaye kugeuka kwa kuume, au kwa kushoto, kukana neno lo lote alilolisema bwana wangu mfalme; kwani mtumwa wako Yoabu ndiye aliyeniamuru, na kuyaweka maneno haya yote kinywani mwa mjakazi wako;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme akamwuliza, “Je, Yoabu anahusika katika jambo hili?” Yule mwanamke akasema, “Kama uishivyo, bwana wangu mfalme, mtu hawezi kukwepa kulia au kushoto kuhusu jambo ulilosema bwana wangu mfalme. Yoabu yule mtumishi wako ndiye aliyenituma. Ni yeye aliyeniambia maneno yote haya niliyokuambia mimi mtumishi wako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akauliza, “Je, mkono wa Yoabu haupo pamoja nawe katika jambo hilo lote?” Huyo mwanamke akajibu, “Hakika kama uishivyo, bwana wangu mfalme, hakuna ye yote anayeweza kugeuka kulia wala kushoto kutokana na cho chote anachosema bwana wangu mfalme. Naam, ni mtumishi wako Yoabu ndiye aliyenifundisha kufanya hivi, naye ndiye aliyeweka maneno haya yote kinywani mwa mtumishi wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akauliza, “Je, mkono wa Yoabu haupo pamoja nawe katika jambo hilo lote?” Huyo mwanamke akajibu, “Hakika kama uishivyo, bwana wangu mfalme, hakuna yeyote anayeweza kugeuka kulia wala kushoto kutokana na chochote anachosema bwana wangu mfalme. Naam, ni mtumishi wako Yoabu ndiye alinifundisha kufanya hivi, naye ndiye aliweka maneno haya yote kinywani mwa mtumishi wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme akasema, Je! Si mkono wa Yoabu ulio pamoja nawe katika haya yote? Mwanamke akajibu, akasema, Kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mfalme, hapana mtu awezaye kugeuka kwa kulia, au kwa kushoto, kukana neno lolote alilolisema bwana wangu mfalme; kwani mtumishi wako Yoabu ndiye aliyeniamuru, na kuyaweka maneno haya yote kinywani mwa mjakazi wako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme akamwuliza, “Je, Yoabu anahusika katika jambo hili?” Yule mwanamke akasema, “Kama uishivyo, bwana wangu mfalme, mtu hawezi kukwepa kulia au kushoto kuhusu jambo ulilosema bwana wangu mfalme. Yoabu yule mtumishi wako ndiye aliyenituma. Ni yeye aliyeniambia maneno yote haya niliyokuambia mimi mtumishi wako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipouliza: Je? Mkono wa Yoabu haumo katika mambo haya yote? Huyu mwanamke akajibu kwamba: Hivyo roho yako, bwana wangu mfalme, ilivyo nzima, hakuna njia kuumeni wala kushotoni ya kupita penye maneno yote, bwana wangu mfalme aliyoyasema; kweli mtumishi wako Yoabu ndiye aliyeniagiza hivyo, naye ndiye aliyeniambia na kinywa chake, kijakazi wako atakayoyasema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akasema, Je! Si mkono wa Yoabu ulio pamoja nawe katika haya yote? Mwanamke akajibu, akasema, Kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mfalme, hapana mtu awezaye kugeuka kwa kuume, au kwa kushoto, kukana neno lo lote alilolisema bwana wangu mfalme; kwani mtumwa wako Yoabu ndiye aliyeniamuru, na kuyaweka maneno haya yote kinywani mwa mjakazi wako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akamwuliza: “Haukupatana na Yoabu katika jambo hili?” Yule mwanamuke akasema: “Kama vile unavyoishi mwenyewe bwana wangu mufalme, mutu hawezi kupita pembeni juu ya jambo ulilosema bwana wangu mufalme. Yoabu yule mutumishi wako ndiye aliyenituma. Ni yeye aliyeniambia maneno yote haya niliyokuambia mimi mujakazi wako.