2 Samuel 14:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika Israeli yote, hakuna yeyote aliyesifiwa kwa uzuri kama Absalomu. Tangu nyayo zake hadi utosini mwake, Absalomu hakuwa na kasoro yoyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika Israeli yote hakuna mtu yeyote aliyesifiwa kwa uzuri wa sura kama Absalomu. Kuanzia utosi wa kichwa chake hadi wayo wa mguu wake hakuwa na kasoro.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi katika Israeli wote hapakuwa na mtu hata mmoja mwenye kusifiwa kwa uzuri wake kama huyo Absalomu; tangu nyayo za miguu yake hata utosi wa kichwa chake hapakuwa na ila kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika Israeli yote, hakuna yeyote aliyesifiwa kwa uzuri kama Absalomu. Tangu nyayo zake hadi utosini mwake, Absalomu hakuwa na kasoro yoyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika Israeli yote hakuna mtu ye yote aliyesifiwa kwa uzuri wa sura kama Absalomu. Kuanzia utosi wa kichwa chake hadi wayo wa mguu wake hapakuwa na kasoro.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika Israeli yote hakuna mtu yeyote aliyesifiwa kwa uzuri wa sura kama Absalomu. Kuanzia utosi wa kichwa chake hadi wayo wa mguu wake hapakuwa na kasoro.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi katika Israeli wote hapakuwa na mtu hata mmoja mwenye kusifiwa kwa uzuri wake kama huyo Absalomu; tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa chake hapakuwa na ila kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika Israeli yote, hakuna yeyote aliyesifiwa kwa uzuri kama Absalomu. Tangu nyayo zake hadi utosini mwake, Absalomu hakuwa na kasoro yoyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwao Waisiraeli wote hakuwako mtu, watu waliyemsifu sana kwa uzuri wake wa mwili kama Abisalomu, toka wayo wa mguu wake mpaka kwenye utosi wake hakikuwako cho chote kisicho kizuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi katika Israeli wote hapakuwa na mtu hata mmoja mwenye kusifiwa kwa uzuri wake kama huyo Absalomu; tangu nyayo za miguu yake hata utosi wa kichwa chake hapakuwa na ila kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika inchi yote ya Israeli, hakuna mutu yeyote aliyesifiwa kwa uzuri wa umbo kama Abusaloma. Tangia kwenye miguu mpaka kwenye kichwa, Abusaloma hakukuwa na kilema chochote.