2 Samuel 14:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila alipokata nywele zake, (na kila mwishoni mwa mwaka alikata nywele zake kwani zilikuwa nzito), alipozipima, zilikuwa na uzito wa kilo mbili kulingana na vipimo vya kifalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mara aliponyoa nywele za kichwa chake, kwa kuwa alizinyoa nywele zake mara moja kwa mwaka kwa sababu zilikuwa nzito sana kwake, alizipima; uzito wake ulikuwa shekeli mia mbili kwa kipimo cha kifalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye aliponyoa kichwa, (basi mwisho wa kila mwaka hunyoa; na kwa sababu nywele zilikuwa nzito kwake, kwa hiyo akanyoa;) hupima nywele za kichwa chake shekeli mia mbili kwa uzani wa mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila alipokata nywele zake, (na kila mwishoni mwa mwaka alikata nywele zake kwani zilikuwa nzito), alipozipima, zilikuwa na uzito wa kilo mbili kulingana na vipimo vya kifalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mara aliponyoa nywele za kichwa chake, kwa kuwa alikuwa akinyoa mara kwa mara zilipokuwa zinamwia nzito, alizipima uzito wake ulikuwa shekeli mia mbili kwa kipimo cha kifalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mara aliponyoa nywele za kichwa chake, kwa kuwa alikuwa akinyoa mara kwa mara zilipokuwa zinamwia nzito, alizipima uzito wake ulikuwa shekeli mia mbili kwa kipimo cha kifalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye aliponyoa kichwa, (basi mwisho wa kila mwaka hunyoa; na kwa sababu nywele zilikuwa nzito kwake, kwa hiyo akanyoa;) hupima nywele za kichwa chake shekeli mia mbili kwa uzani wa mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila alipokata nywele zake, (na kila mwishoni mwa mwaka alikata nywele zake kwani zilikuwa nzito), alipozipima, zilikuwa na uzito wa kilo mbili kulingana na vipimo vya kifalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kila mara siku za mwaka mmoja zilipopita akazinyoa nywele za kichwani, naye huzinyoa, zikimlemea kwa uzito; tena alipokwisha kuzinyoa huzipima hizo nywele za kichwani pake, nazo huwa kama sekeli 200, ndio ratli 7 kwa kipimo cha mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye aliponyoa kichwa, (basi mwisho wa kila mwaka hunyoa; na kwa sababu nywele zilikuwa nzito kwake, kwa hiyo akanyoa;) hupima nywele za kichwa chake shekeli mia mbili kwa uzani wa mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mara alipokata nywele zake, (na kila mwisho wa mwaka alikata nywele zake maana zilikuwa nzito), alipozipima, zilikuwa na uzito wa kilo mbili kulingana na vipimo vya kifalme.