2 Samuel 14:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Absalomu alimtumia ujumbe Yoabu, ili aende kwa mfalme kwa niaba yake, lakini Yoabu akakataa. Absalomu akatuma ujumbe mara ya pili lakini Yoabu akakataa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Absalomu akamtumania Yoabu kwa kusudi la kumtuma kwa mfalme, lakini Yoabu akakataa kuja kwa Absalomu. Ndipo akamtumania mara ya pili, lakini pia akakataa kuja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Absalomu akatuma kumwita Yoabu, ampeleke kwa mfalme, lakini yeye akakataa kumjia; akatuma tena mara ya pili, lakini akakataa kuja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Absalomu alimtumia ujumbe Yoabu, ili aende kwa mfalme kwa niaba yake, lakini Yoabu akakataa. Absalomu akatuma ujumbe mara ya pili lakini Yoabu akakataa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Absalomu akamwita Yaobu kwa kusudi la kumtuma kwa mfalme, lakini Yoabu akakataa kuja kwa Absalomu. Ndipo akamwita tena mara ya pili, lakini pia akakataa kuja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Absalomu akamwita Yoabu kwa kusudi la kumtuma kwa mfalme, lakini Yoabu akakataa kuja kwa Absalomu. Ndipo akamwita tena mara ya pili, lakini pia akakataa kuja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Absalomu akatuma Yoabu aitwe, amtume kwa mfalme, lakini yeye akakataa kumjia; akatuma tena mara ya pili, lakini akakataa kuja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Absalomu alimtumia ujumbe Yoabu, ili aende kwa mfalme kwa niaba yake, lakini Yoabu akakataa. Absalomu akatuma ujumbe mara ya pili lakini Yoabu akakataa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, Abisalomu alipotuma kwa Yoabu, apate kumtuma kwa mfalme, lakini akakataa kufika kwake. Akatuma tena mara ya pili, lakini akakataa kufika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Absalomu akatuma kumwita Yoabu, ampeleke kwa mfalme, lakini yeye akakataa kumjia; akatuma tena mara ya pili, lakini akakataa kuja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Abusaloma alimutumia Yoabu ujumbe, kusudi aende kwa mufalme kwa jina lake, lakini Yoabu akakataa. Abusaloma akatuma ujumbe mara ya pili lakini Yoabu akakataa.