2 Samuel 15:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Absalomu alituma wajumbe kwa siri katika makabila yote ya Israeli, wakasema, “Mara moja mtakaposikia mlio wa tarumbeta, semeni, ‘Absalomu ni mfalme katika Hebroni!’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Absalomu akatuma wajumbe kwa siri katika makabila yote ya Israeli, kusema, “Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta basi semeni, ‘Absalomu ni mfalme huko Hebroni.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Absalomu akapeleka wapelelezi katika kabila zote za Israeli kusema, Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta, ndipo mtakaposema Absalomu anamilikl huko Hebroni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Absalomu alituma wajumbe kwa siri katika makabila yote ya Israeli, wakasema, “Mara moja mtakaposikia mlio wa tarumbeta, semeni, ‘Absalomu ni mfalme katika Hebroni!’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Absalomu akatuma wajumbe kwa siri katika makabila yote ya Israeli, kusema, “Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta basi semeni, ‘Absalomu ni mfalme huko Hebroni.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Absalomu akatuma wajumbe kwa siri katika makabila yote ya Israeli, kusema, “Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta basi semeni, ‘Absalomu ni mfalme huko Hebroni.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Absalomu akatuma wapelelezi katika kabila zote za Israeli kusema, Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta, ndipo mtakaposema Absalomu anatawala huko Hebroni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Absalomu alituma wajumbe kwa siri katika makabila yote ya Israeli, wakasema, “Mara moja mtakaposikia mlio wa tarumbeta, semeni, ‘Absalomu ni mfalme katika Hebroni!’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Abisalomu akatuma wapelelezi kwa mashina yote ya Waisiraeli kwamba: Mtakaposikia, mabaragumu yakilia, semeni: Abisalomu amepata ufalme Heburoni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Absalomu akapeleka wapelelezi katika kabila zote za Israeli kusema, Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta, ndipo mtakaposema Absalomu anamilikl huko Hebroni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Abusaloma alituma wajumbe kwa siri katika makabila yote ya Waisraeli, wakasema: “Mara moja mutakaposikia mulio wa baragumu, museme: ‘Abusaloma ni mufalme katika Hebroni!’ ”