2 Samuel 15:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati Absalomu alipokuwa akitoa tambiko, alituma ujumbe mjini Gilo kumwita Ahithofeli, Mgilo, aliyekuwa mshauri wa mfalme Daudi. Uasi wa Absalomu ukazidi kupata nguvu na watu walioandamana naye wakazidi kuongezeka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Absalomu alipokuwa anatoa dhabihu, pia akatuma aitwe Ahithofeli Mgiloni, mshauri wa Daudi, aje kutoka Gilo, ambao ndio mji wake wa nyumbani. Kwa hiyo mpango wa hila ukapata nguvu, na idadi ya waliofuatana na Absalomu ikaongezeka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Absalomu naye akatuma kumwita Ahithofeli Mgiloni, mshauri wake Daudi, kutoka katika mji wake, yaani, Gilo, alipokuwa akitoa dhabihu. Fitina yao ikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu wakazidi kuwa wengi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati Absalomu alipokuwa akitoa tambiko, alituma ujumbe mjini Gilo kumwita Ahithofeli, Mgilo, aliyekuwa mshauri wa mfalme Daudi. Uasi wa Absalomu ukazidi kupata nguvu na watu walioandamana naye wakazidi kuongezeka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Absalomu alipokuwa anatoa dhabihu, pia akatuma aitwe Ahithofeli, Mgiloni, mshauri wa Daudi, aje kutoka Gilo, ambao ndio mji wake wa nyumbani. Kwa hiyo mpango wa hila ukapata nguvu, na idadi ya waliofuatana na Absalomu ikaongezeka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Absalomu alipokuwa anatoa dhabihu, pia akatuma aitwe Ahithofeli, Mgiloni, mshauri wa Daudi, aje kutoka Gilo, ambao ndio mji wake wa nyumbani. Kwa hiyo mpango wa hila ukapata nguvu, na idadi ya waliofuatana na Absalomu ikaongezeka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Absalomu alipokuwa akitoa dhabihu alituma Ahithofeli Mgiloni, Mshauri wake Daudi, aitwe kutoka mji wake, yaani, Gilo. Njama zao zikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu walizidi kuongezeka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati Absalomu alipokuwa akitoa tambiko, alituma ujumbe mjini Gilo kumwita Ahithofeli, Mgilo, aliyekuwa mshauri wa mfalme Daudi. Uasi wa Absalomu ukazidi kupata nguvu na watu walioandamana naye wakazidi kuongezeka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Abisalomu akatuma kumchukua Ahitofeli wa Gilo aliyekuwa mmoja wao waliomwongoza Dawidi mashaurini; akamtoa huko Gilo mjini kwake, alipochinja ng'ombe za tambiko. Hivyo lile fujo likapata nguvu, nao watu waliorudi upande wa Abisalomu wakaendelea kuwa wengi zaidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Absalomu naye akatuma kumwita Ahithofeli Mgiloni, mshauri wake Daudi, kutoka katika mji wake, yaani, Gilo, alipokuwa akitoa dhabihu. Fitina yao ikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu wakazidi kuwa wengi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Abusaloma alipokuwa akitoa sadaka, alituma ujumbe katika muji wa Gilo kwa kumwita Ahitofeli wa muji wa Gilo, aliyekuwa mushauri wa mufalme Daudi. Uasi wa Abusaloma ukazidi kupata nguvu na watu waliojiunga naye wakazidi kuongezeka.