2 Samuel 15:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, Daudi aliambiwa kuwa hata Ahithofeli alikuwa mmoja wa waasi waliojiunga na Absalomu. Lakini Daudi akaomba akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu nakuomba, uufanye mpango wa Ahithofeli usifanikiwe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Daudi alikuwa ameambiwa, “Ahithofeli alikuwa miongoni mwa washiriki wa njama ya Absalomu.” Ndipo Daudi akaomba, akisema, “Ee Mwenyezi Mungu, geuza ushauri wa Ahithofeli kuwa ujinga.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee Bwana, nakusihi, uligeuze shauri la Ahithofeli liwe ubatili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, Daudi aliambiwa kuwa hata Ahithofeli alikuwa mmoja wa waasi waliojiunga na Absalomu. Lakini Daudi akaomba akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu nakuomba, uufanye mpango wa Ahithofeli usifanikiwe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Daudi alikuwa ameambiwa, “Ahithofeli alikuwa miongoni mwa washiriki wa shauri baya la Absalomu.” Ndipo Daudi akaomba, akisema, “Ee BWANA, geuza shauri la Ahithofeli kuwa ujinga.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Daudi alikuwa ameambiwa, “Ahithofeli alikuwa miongoni mwa washiriki wa shauri baya la Absalomu.” Ndipo Daudi akaomba, akisema, “Ee bwana, geuza shauri la Ahithofeli kuwa ujinga.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, Daudi aliambiwa kuwa hata Ahithofeli alikuwa mmoja wa waasi waliojiunga na Absalomu. Lakini Daudi akaomba akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu nakuomba, uufanye mpango wa Ahithofeli usifanikiwe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipompasha Dawidi habari ya kwamba: Ahitofeli yuko kwa Abisalomu pamoja nao waliovunja maagano, Dawidi akasema: Bwana na aligeuze shauri la Ahitofeli kuwa ujinga!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uligeuze shauri la Ahithofeli liwe ubatili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule, Daudi aliambiwa kwamba hata Ahitofeli alikuwa mumoja wa waasi waliojiunga na Abusaloma. Lakini Daudi akaomba akisema: “Ee Yawe, ninakuomba uyafanye mashauri ya Ahitofeli yasifanikiwe.”