2 Samuel 15:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi alipofika kwenye kilele cha mlima, mahali pa kumwabudia Mungu, mtu mmoja jina lake Hushai kutoka Arki alikuja ili kumlaki, mavazi yake yakiwa yameraruka na kichwani pake kuna mavumbi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi alipofika kwenye kilele cha mlima, mahali watu walikuwa wamezoea kumwabudu Mungu, Hushai Mwarki alikuwako kumlaki, akiwa amerarua joho lake, na akiwa na mavumbi kichwani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, Daudi alipofika juu, hapo Mungu alipoabudiwa, tazama, Hushai, Mwarki, akaja kumlaki na joho lake limeraruliwa, tena ana udongo kichwani mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi alipofika kwenye kilele cha mlima, mahali pa kumwabudia Mungu, mtu mmoja jina lake Hushai kutoka Arki alikuja ili kumlaki, mavazi yake yakiwa yameraruka na kichwani pake kuna mavumbi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi alipofika kwenye kilele cha mlima, mahali ambapo watu walikuwa wamezoea kumwabudu Mungu, Hushai, Mwarki, alikuwako huko kumlaki, joho lake likiwa limeraruka na mavumbi kichwani mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi alipofika kwenye kilele cha mlima, mahali ambapo watu walikuwa wamezoea kumwabudu Mungu, Hushai, Mwariki, alikuwako huko kumlaki, joho lake likiwa limeraruka na mavumbi kichwani mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, Daudi alipofika juu, hapo Mungu alipoabudiwa, tazama, Hushai, Mwarki, akaja kumlaki na joho lake likiwa limeraruliwa, tena akiwa na udongo kichwani mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi alipofika kwenye kilele cha mlima, mahali pa kumwabudia Mungu, mtu mmoja jina lake Hushai kutoka Arki alikuja ili kumlaki, mavazi yake yakiwa yameraruka na kichwani pake kuna mavumbi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi alipofika pale juu, watu wanapomtambikia Mungu, mara akaja Mwarki Husai akimwendea njiani mwenye kanzu iliyoraruliwa na mwenye mchanga kichwani pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, Daudi alipofika juu, hapo Mungu alipoabudiwa, tazama, Hushai, Mwarki, akaja kumlaki na joho lake limeraruliwa, tena ana udongo kichwani mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi alipofika kwenye kichwa cha mulima, nafasi ya kumwabudia Mungu, mutu mumoja jina lake Husai kutoka inchi ya Arki alikuja kwa kumupokea, nguo zake zikiwa zimepasuka na juu ya kichwa chake kuna mavumbi.