2 Samuel 15:34 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama utarudi mjini Yerusalemu na kumwambia Absalomu, ‘Nitakuwa mtumishi wako, ee mfalme; kama vile nilivyokuwa mtumishi wa baba yako, hapo awali’; basi utanifanyia mpango wa Ahithofeli usifanikiwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ukirudi mjini na kumwambia Absalomu, ‘Nitakuwa mtumishi wako, ee mfalme; nilikuwa mtumishi wa baba yako wakati uliopita, lakini sasa nitakuwa mtumishi wako,’ basi utaweza kunisaidia kwa kupinga ushauri wa Ahithofeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini ukirudi mjini, na kumwambia Absalomu, Nitakuwa mtumishi wako, Ee mfalme; kama vile nilivyokuwa mtumishi wa baba yako tokea zamani, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako sasa; ndipo utayavunja mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama utarudi mjini Yerusalemu na kumwambia Absalomu, ‘Nitakuwa mtumishi wako, ee mfalme; kama vile nilivyokuwa mtumishi wa baba yako, hapo awali’; basi utanifanyia mpango wa Ahithofeli usifanikiwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ikiwa utarudi mjini na kumwambia Absalomu, ‘Nitakuwa mtumishi wako, Ee mfalme; nilikuwa mtumishi wa baba yako wakati uliopita, lakini sasa nitakuwa mtumishi wako,’ basi utaweza kunisaidia kwa kupinga shauri la Ahithofeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ikiwa utarudi mjini na kumwambia Absalomu, ‘Nitakuwa mtumishi wako, ee mfalme; nilikuwa mtumishi wa baba yako wakati uliopita, lakini sasa nitakuwa mtumishi wako,’ basi utaweza kunisaidia kwa kupinga shauri la Ahithofeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini ukirudi mjini, na kumwambia Absalomu, Nitakuwa mtumishi wako, Ee mfalme; kama vile nilivyokuwa mtumishi wa baba yako tokea zamani, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako sasa; ndipo utayavunja mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama utarudi mjini Yerusalemu na kumwambia Absalomu, ‘Nitakuwa mtumishi wako, ee mfalme; kama vile nilivyokuwa mtumishi wa baba yako, hapo awali’; basi utanifanyia mpango wa Ahithofeli usifanikiwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ukirudi mjini na kumwambia Abisalomu: Mimi nitakuwa mtumishi wako, mfalme; kama nilivyokuwa mtumishi wa baba yako tangu kale, ndivyo, nitakavyokuwa sasa mtumishi wako. Basi, ndivyo, utakavyolitengua shauri la Ahitofeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini ukirudi mjini, na kumwambia Absalomu, Nitakuwa mtumishi wako, Ee mfalme; kama vile nilivyokuwa mtumishi wa baba yako tokea zamani, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako sasa; ndipo utayavunja mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Urudi Yerusalema na kumwambia Abusaloma: ‘Nitakuwa mutumishi wako, ee mufalme, kama vile nilivyokuwa zamani mutumishi wa baba yako’. Kwa njia hiyo utanisaidia kupinga mashauri ya Ahitofeli.