2 Samuel 15:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
maana, mimi mtumishi wako, nilipoishi kule Geshuri katika Aramu, nilimwekea Mwenyezi-Mungu nadhiri nikisema kuwa kama Mwenyezi-Mungu atanirudisha mjini Yerusalemu basi, nitamwabudu yeye.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtumishi wako alipokuwa huko Geshuri katika nchi ya Aramu, niliweka nadhiri hii: ‘Ikiwa Mwenyezi Mungu atanirudisha Yerusalemu, nitamwabudu Mwenyezi Mungu huko Hebroni.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mimi mtumishi wako naliweka nadhiri hapo nilipokuwa nikikaa Geshuri katika Shamu, nikasema, Kama Bwana akinirudisha Yerusalemu kweli, ndipo nitamtumikia Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
maana, mimi mtumishi wako, nilipoishi kule Geshuri katika Aramu, nilimwekea Mwenyezi-Mungu nadhiri nikisema kuwa kama Mwenyezi-Mungu atanirudisha mjini Yerusalemu basi, nitamwabudu yeye.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mtumishi wako alipokuwa huko Geshuri katika nchi ya Aramu, niliweka nadhiri hii, ‘Ikiwa BWANA atanirudisha Yerusalemu, nitamwabudu BWANA huko Hebroni.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati mtumishi wako alipokuwa huko Geshuri katika nchi ya Aramu, niliweka nadhiri hii, ‘Ikiwa bwana atanirudisha Yerusalemu, nitamwabudu bwana huko Hebroni.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mimi mtumishi wako niliweka nadhiri hapo nilipokuwa nikikaa Geshuri katika Shamu, nikasema, Kama BWANA akinirudisha Yerusalemu kweli, ndipo nitamtumikia BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
maana, mimi mtumishi wako, nilipoishi kule Geshuri katika Aramu, nilimwekea Mwenyezi-Mungu nadhiri nikisema kuwa kama Mwenyezi-Mungu atanirudisha mjini Yerusalemu basi, nitamwabudu yeye.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mtumishi wako ameapa kiapo, nilipokaa Gesuri kwa Washami, cha kwamba: Kama Bwana atanirudisha Yerusalemu, nitamtumikia Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mimi mtumishi wako naliweka nadhiri hapo nilipokuwa nikikaa Geshuri katika Shamu, nikasema, Kama BWANA akinirudisha Yerusalemu kweli, ndipo nitamtumikia BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana, mimi mutumishi wako, nilipoishi kule Gesuri katika inchi ya Aramu, nilimufanyia Yawe kiapo nikisema kama Yawe akinirudisha Yerusalema basi, nitamwabudu yeye.”