2 Samuel 16:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ahithofeli akamwambia Absalomu, “Waingilie masuria wa baba yako ambao aliwaacha kuangalia nyumba yake. Baadaye watu wote wa Israeli watakaposikia kwamba umechukizwa na baba yako, hapo watu wote walio pamoja nawe watatiwa nguvu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ahithofeli akamjibu Absalomu, “Kutana kimwili na masuria wa baba yako aliowaacha kutunza jumba la kifalme. Ndipo Israeli yote itakaposikia kwamba umejifanya chukizo kwa baba yako, nayo mikono ya kila mmoja aliye pamoja nawe itatiwa nguvu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Ahithofeli akamwambia Absalomu, Ingia wewe kwa masuria ya baba yako, hao aliowaacha ili kutunza nyumba; na Israeli wote watasikia ya kuwa umechukizwa kabisa na baba yako; ndipo itatiwa nguvu mikono yao wote walio pamoja nawe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ahithofeli akamwambia Absalomu, “Waingilie masuria wa baba yako ambao aliwaacha kuangalia nyumba yake. Baadaye watu wote wa Israeli watakaposikia kwamba umechukizwa na baba yako, hapo watu wote walio pamoja nawe watatiwa nguvu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ahithofeli akajibu, “Kutana kimwili na masuria wa baba yako aliowaacha kuangalia jumba la kifalme. Ndipo Israeli yote itakaposikia kwamba umejifanya chukizo kwa baba yako, nayo mikono ya kila mmoja aliye pamoja nawe itatiwa nguvu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ahithofeli akamjibu, “Kutana kimwili na masuria wa baba yako aliowaacha kutunza jumba la kifalme. Ndipo Israeli yote itakaposikia kwamba umejifanya chukizo kwa baba yako, nayo mikono ya kila mmoja aliye pamoja nawe itatiwa nguvu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Ahithofeli akamwambia Absalomu, Ingia wewe kwa masuria wa baba yako, hao aliowaacha ili kutunza nyumba; na Israeli wote watasikia ya kuwa umechukizwa kabisa na baba yako; ndipo itatiwa nguvu mikono yao wote walio pamoja nawe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ahithofeli akamwambia Absalomu, “Waingilie masuria wa baba yako ambao aliwaacha kuangalia nyumba yake. Baadaye watu wote wa Israeli watakaposikia kwamba umechukizwa na baba yako, hapo watu wote walio pamoja nawe watatiwa nguvu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ahitofeli akamwambia Abisalomu: Ingia kwao masuria wa baba yako, aliowaacha kuiangalia nyumba! Hapo, Waisiraeli wote watakaposikia, ya kuwa umechukizwa kabisa na baba yako, ndipo, mikono yao wote waliorudi upande wako itakapopata nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Ahithofeli akamwambia Absalomu, Ingia wewe kwa masuria ya baba yako, hao aliowaacha ili kutunza nyumba; na Israeli wote watasikia ya kuwa umechukizwa kabisa na baba yako; ndipo itatiwa nguvu mikono yao wote walio pamoja nawe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ahitofeli akamwambia Abusaloma: “Ulale na wale wahabara za baba yako ambao aliwaacha kuangalia nyumba yake. Kisha watu wote wa Israeli watakaposikia kwamba umechukizwa na baba yako, hapo watu wote wanaokuwa pamoja nawe watapata nguvu.”