2 Samuel 17:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nasi tutamwendea Daudi mahali popote anapoweza kupatikana na tutamvamia kama umande unavyoiangukia ardhi. Basi, hakuna atakayesalia hata kama atakuwa yeye mwenyewe au watu wake wote walio pamoja naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo tutakapomshambulia popote atakapoonekana, nasi tutamwangukia kama umande unavyoshuka juu ya ardhi. Yeye mwenyewe na watu wake hakuna atakayeachwa hai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo tutamfikia mahali po pote atakapoonekana, na kumwangukia kama vile umande uangukavyo juu ya nchi; wala hatutaacha hata mmoja wao, yeye na watu wote walio pamoja naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nasi tutamwendea Daudi mahali popote anapoweza kupatikana na tutamvamia kama umande unavyoiangukia ardhi. Basi, hakuna atakayesalia hata kama atakuwa yeye mwenyewe au watu wake wote walio pamoja naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo tutakapomshambulia po pote atakapoonekana, nasi tutamwangukia kama umande unavyoshuka juu ya ardhi. Yeye mwenyewe wala watu wake hakuna atakayeachwa hai.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo tutakapomshambulia popote atakapoonekana, nasi tutamwangukia kama umande unavyoshuka juu ya ardhi. Yeye mwenyewe wala watu wake hakuna atakayeachwa hai.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo tutamfikia mahali popote atakapoonekana, na kumwangukia kama vile umande uangukavyo juu ya nchi; wala hatutaacha hata mmoja wao, yeye na watu wote walio pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nasi tutamwendea Daudi mahali popote anapoweza kupatikana na tutamvamia kama umande unavyoiangukia ardhi. Basi, hakuna atakayesalia hata kama atakuwa yeye mwenyewe au watu wake wote walio pamoja naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha tutamshambulia mahali pamoja; atakapoonekana, tumwangukie, kama umande unavyoiangukia nchi, tusisaze kwake hata mtu mmoja miongoni mwao wote waliokuwa naye!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo tutamfikia mahali po pote atakapoonekana, na kumwangukia kama vile umande uangukavyo juu ya nchi; wala hatutaacha hata mmoja wao, yeye na watu wote walio pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nasi tutamwendea Daudi pahali popote anapoweza kupatikana na tutamwangukia sawa vile umande unavyoanguka juu ya udongo. Basi, hakuna atakayebakia hata kama ni yeye mwenyewe au watu wake wote wanaokuwa pamoja naye.