2 Samuel 17:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Absalomu pamoja na watu wote wa Israeli wakasema, “Shauri la Hushai ni bora kuliko shauri la Ahithofeli.” Wakakataa shauri la Ahithofeli kwa kuwa Mwenyezi-Mungu alikuwa amepanga kulishinda shauri jema la Ahithofeli ili aweze kumletea Absalomu maafa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Absalomu na wanaume wote wa Israeli wakasema, “Ushauri wa Hushai, Mwarki, ni mwema kuliko ule wa Ahithofeli.” Kwa maana Mwenyezi Mungu alikuwa amekusudia kupinga ushauri mwema wa Ahithofeli, ili kuleta maafa kwa Absalomu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Shauri la Hushai, Mwarki, ni jema kuliko shauri la Ahithofeli. Kwa maana Bwana alikuwa amekusudia kulivunja shauri jema la Ahithofeli, ili Bwana alete mabaya juu ya Absalomu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Absalomu pamoja na watu wote wa Israeli wakasema, “Shauri la Hushai ni bora kuliko shauri la Ahithofeli.” Wakakataa shauri la Ahithofeli kwa kuwa Mwenyezi-Mungu alikuwa amepanga kulishinda shauri jema la Ahithofeli ili aweze kumletea Absalomu maafa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, “Shauri la Hushai, Mwarki, ni jema zaidi kuliko lile la Ahithofeli.” Kwa maana BWANA alikuwa amekusudia kupinga shauri nzuri la Ahithofeli, ili kuleta maafa juu ya Absalomu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, “Shauri la Hushai, Mwariki, ni jema zaidi kuliko lile la Ahithofeli.” Kwa maana bwana alikuwa amekusudia kupinga shauri nzuri la Ahithofeli, ili kuleta maafa juu ya Absalomu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Ushauri wa Hushai, Mwarki, ni mwema kuliko ushauri wa Ahithofeli. Kwa maana BWANA alikuwa amekusudia kuuvunja ushauri mwema wa Ahithofeli, ili BWANA alete mabaya juu ya Absalomu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Absalomu pamoja na watu wote wa Israeli wakasema, “Shauri la Hushai ni bora kuliko shauri la Ahithofeli.” Wakakataa shauri la Ahithofeli kwa kuwa Mwenyezi-Mungu alikuwa amepanga kulishinda shauri jema la Ahithofeli ili aweze kumletea Absalomu maafa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Abisalomu na watu wote wa Waisiraeli waliposema: Shauri la Mwarki Husai ni jema kuliko shauri la Ahitofeli. Lakini alikuwa Bwana aliyeagiza kulitengua shauri jema la Ahitofeli, kusudi Bwana ampatie Abisalomu mabaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Shauri la Hushai, Mwarki, ni jema kuliko shauri la Ahithofeli. Kwa maana BWANA alikuwa amekusudia kulivunja shauri jema la Ahithofeli, ili BWANA alete mabaya juu ya Absalomu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Abusaloma pamoja na watu wote wa Israeli wakasema: “Shauri la Husayi ni bora kuliko shauri la Ahitofeli.” Wakakataa shauri la Ahitofeli kwa sababu Yawe alikuwa amepanga kulishinda shauri jema la Ahitofeli kusudi aweze kumuletea Abusaloma hasara.