2 Samuel 17:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya watumishi wa Absalomu kuondoka, Yonathani na Ahimaasi walitoka kisimani, wakaenda kwa mfalme Daudi na kumpasha habari. Wakamwambia, “Ondoka, uende ngambo ya mto, kwa sababu Ahithofeli amemshauri Absalomu dhidi yako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya watu hao kuondoka, wale watu wawili yaani Yonathani na Ahimaasi wakapanda kutoka mle kisimani na kwenda kumpasha Mfalme Daudi habari. Wakamwambia, “Ondoka, uvuke mto haraka. Ahithofeli ameshauri hivi na hivi dhidi yako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha ikawa, baada ya kuondoka kwao, wale wakatoka kisimani, wakaenda wakamwarifu mfalme Daudi; wakamwambia Daudi, Ondokeni, mkavuke maji haya upesi; maana ndivyo alivyotoa shauri Ahithofeli juu yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya watumishi wa Absalomu kuondoka, Yonathani na Ahimaasi walitoka kisimani, wakaenda kwa mfalme Daudi na kumpasha habari. Wakamwambia, “Ondoka, uende ng'ambo ya mto, kwa sababu Ahithofeli amemshauri Absalomu dhidi yako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya watu hao kuondoka, wale watu wawili yaani Yonathani na Ahimaasi wakapanda kutoka mle kisimani na kwenda kumpasha Mfalme Daudi habari. Wakamwambia, “Ondoka, uvuke haya maji haraka. Ahithofeli ameshauri kadha wa kadha dhidi yako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya watu hao kuondoka, wale watu wawili yaani Yonathani na Ahimaasi wakapanda kutoka mle kisimani na kwenda kumpasha Mfalme Daudi habari. Wakamwambia, “Ondoka, uvuke haya maji haraka. Ahithofeli ameshauri kadha wa kadha dhidi yako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha ikawa, baada ya kuondoka kwao, wale wakatoka kisimani, wakaenda wakamwarifu mfalme Daudi; wakamwambia Daudi, Ondokeni, mkavuke maji haya upesi; maana ndivyo alivyotoa shauri Ahithofeli juu yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya watumishi wa Absalomu kuondoka, Yonathani na Ahimaasi walitoka kisimani, wakaenda kwa mfalme Daudi na kumpasha habari. Wakamwambia, “Ondoka, uende ngambo ya mto, kwa sababu Ahithofeli amemshauri Absalomu dhidi yako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hao walipokwisha kwenda, wale wakatoka kisimani, wakaenda kumpasha mfalme Dawidi habari, wakamwambia Dawidi: Ondokeni, mvuke upesi mtoni! Kwani haya ndiyo mashauri, Ahitofeli aliyoyatoa kwa ajili yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha ikawa, baada ya kuondoka kwao, wale wakatoka kisimani, wakaenda wakamwarifu mfalme Daudi; wakamwambia Daudi, Ondokeni, mkavuke maji haya upesi; maana ndivyo alivyotoa shauri Ahithofeli juu yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya watumishi wa Abusaloma kuondoka, Yonatani na Ahimasi walitoka ndani ya kisima, wakaenda kwa mufalme Daudi na kumupasha habari. Wakamwambia: “Ondoka, uende ngambo ya muto, kwa sababu Ahitofeli amemushauria Abusaloma juu yako.”