2 Samuel 17:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ahithofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, alitandika punda wake, akaenda nyumbani, kwenye mji wake. Alipofika huko, alipanga vizuri mambo ya nyumbani kwake, akajinyonga. Akafariki na kuzikwa kwenye kaburi la baba yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ahithofeli alipoona kwamba ushauri wake haukufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka kwenda nyumbani mwake kwenye mji wake. Akaiweka nyumba yake katika utaratibu, kisha akajinyonga mwenyewe. Hivyo akafa na akazikwa katika kaburi la baba yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajisonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ahithofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, alitandika punda wake, akaenda nyumbani, kwenye mji wake. Alipofika huko, alipanga vizuri mambo ya nyumbani kwake, akajinyonga. Akafariki na kuzikwa kwenye kaburi la baba yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ahithofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka kwenda nyumbani kwake kwenye mji wake. Akaiweka nyumba yake katika utaratibu, kisha akajinyonga mwenyewe. Hivyo akafa na akazikwa katika kaburi la baba yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ahithofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka kwenda nyumbani kwake kwenye mji wake. Akaiweka nyumba yake katika utaratibu, kisha akajinyonga mwenyewe. Hivyo akafa na akazikwa katika kaburi la baba yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa ushauri wake haukufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajinyonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ahithofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, alitandika punda wake, akaenda nyumbani, kwenye mji wake. Alipofika huko, alipanga vizuri mambo ya nyumbani kwake, akajinyonga. Akafariki na kuzikwa kwenye kaburi la baba yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ahitofeli alipoona, ya kuwa shauri lake halikufanywa, akamtandika punda wake, akaondoka kwenda nyumbani mjini kwake, akayatengeneza mambo ya nyumbani, kisha akajinyonga, akafa, akazikwa kaburini mwa baba yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajisonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ahitofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, alitandika punda wake, akaenda kwake, kwenye muji wake. Alipofika kule, alipanga vizuri mambo ya nyumba yake, akajitundika. Akakufa na kuzikwa kwenye kaburi la baba yake.