2 Samuel 17:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, Absalomu alikuwa amemweka Amasa kuwa mkuu wa jeshi badala ya Yoabu. Amasa alikuwa mwana wa Yithra, Mwishmaeli. Mama yake aliitwa Abigali binti wa Nahashi, aliyekuwa dada yake, Seruya, mama yake Yoabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Absalomu alikuwa amemweka Amasa awe mkuu wa jeshi badala ya Yoabu. Amasa alikuwa mwana wa mtu mmoja aliyeitwa Yetheri, Mwishmaeli aliyekuwa amemwoa Abigaili binti Nahashi, dada yake Seruya mamaye Yoabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Absalomu akamweka Amasa awe juu ya jeshi mahali pa Yoabu. Basi huyo Amasa alikuwa mwana wa mtu, jina lake Yetheri, Mwishmaeli, aliyeingia kwa Abigali, binti Nahashi, nduguye Seruya, mamaye Yoabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, Absalomu alikuwa amemweka Amasa kuwa mkuu wa jeshi badala ya Yoabu. Amasa alikuwa mwana wa Yithra, Mwishmaeli. Mama yake aliitwa Abigali binti wa Nahashi, aliyekuwa dada yake, Seruya, mama yake Yoabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Absalomu alikuwa amemweka Amasa juu ya jeshi badala ya Yoabu. Amasa alikuwa mwana wa mtu mmoja aliyeitwa Yetheri, Mwishmaeli, ambaye alikuwa amemwoa Abigaili binti Nahashi, dada yake Seruya mamaye Yaobu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Absalomu alikuwa amemweka Amasa juu ya jeshi badala ya Yoabu. Amasa alikuwa mwana wa mtu mmoja aliyeitwa Yetheri, Mwisraeli, ambaye alikuwa amemwoa Abigaili binti Nahashi, dada yake Seruya mamaye Yoabu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Absalomu akamweka Amasa awe juu ya jeshi mahali pa Yoabu. Basi huyo Amasa alikuwa mwana wa mtu, jina lake Yetheri, Mwishmaeli, aliyeingia kwa Abigali, binti Nahashi, nduguye Seruya, mamaye Yoabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, Absalomu alikuwa amemweka Amasa kuwa mkuu wa jeshi badala ya Yoabu. Amasa alikuwa mwana wa Yithra, Mwishmaeli. Mama yake aliitwa Abigali binti wa Nahashi, aliyekuwa dada yake, Seruya, mama yake Yoabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Abisalomu alimweka Amasa kuwa mkuu wa vikosi mahali pake Yoabu; Amasa alikuwa mwana wa mtu aitwaye Itira wa Isiraeli; ndiye aliyeingia kale kwa Abigaili, binti Nahasi, umbu la Seruya aliyekuwa mama yake Yoabu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Absalomu akamweka Amasa awe juu ya jeshi mahali pa Yoabu. Basi huyo Amasa alikuwa mwana wa mtu, jina lake Yetheri, Mwishmaeli, aliyeingia kwa Abigali, binti Nahashi, nduguye Seruya, mamaye Yoabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule, Abusaloma alikuwa amemuweka Amasa kuwa jemadari wa waaskari pahali pa Yoabu. Amasa alikuwa mwana wa Itira, Mwisimaeli. Mama yake aliitwa Abigaili binti wa Nahasi, aliyekuwa dada ya Zeruya mama ya Yoabu.