2 Samuel 17:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata sasa amekwisha jificha kwenye mojawapo ya mapango yaliyoko huko au mahali pengine. Mtu yeyote atakayesikia kuuawa kwa watu katika mashambulizi ya kwanza atasema kuwa mauaji yametokea katika kundi la wafuasi wa Absalomu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata sasa, amefichwa ndani ya pango au mahali pengine. Kama atatangulia kushambulia vikosi vyako, yeyote asikiaye habari hii atasema, ‘Kuna machinjo makubwa miongoni mwa vikosi vinavyomfuata Absalomu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Angalia, amefichwa sasa katika shimo, au penginepo; kisha itakuwa, watakapoanguka baadhi yao mwanzo, kila mtu atakayesikia, atasema, Kuna machinjo katika watu wanaofuatana na Absalomu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata sasa amekwisha jificha kwenye mojawapo ya mapango yaliyoko huko au mahali pengine. Mtu yeyote atakayesikia kuuawa kwa watu katika mashambulizi ya kwanza atasema kuwa mauaji yametokea katika kundi la wafuasi wa Absalomu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata sasa, amefichwa ndani ya pango au mahali pengine. Kama atatangulia kushambulia vikosi vyako, ye yote asikiaye habari hii atasema, ‘Kuna machinjo makubwa miongoni mwa vikosi vinavyomfuata Absalomu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata sasa, amefichwa ndani ya pango au mahali pengine. Kama atatangulia kushambulia vikosi vyako, yeyote asikiaye habari hii atasema, ‘Kuna machinjo makubwa miongoni mwa vikosi vinavyomfuata Absalomu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Angalia, amefichwa sasa katika shimo, au penginepo; kisha itakuwa, watakapoanguka baadhi yao mwanzo, kila mtu atakayesikia, atasema, Kuna mauaji katika watu wanaofuatana na Absalomu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata sasa amekwisha jificha kwenye mojawapo ya mapango yaliyoko huko au mahali pengine. Mtu yeyote atakayesikia kuuawa kwa watu katika mashambulizi ya kwanza atasema kuwa mauaji yametokea katika kundi la wafuasi wa Absalomu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama, sasa yeye amekwisha kujificha katika shimo moja au penginepo palipo hivyo; lakini itakapokuwa, mwanzoni watu wa kwetu wauawe kwa kupigana nao, kila atakayevisikia atasema: Watu wanaomfuata Abisalomu wameshindwa katika mapigano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Angalia, amefichwa sasa katika shimo, au penginepo; kisha itakuwa, watakapoanguka baadhi yao mwanzo, kila mtu atakayesikia, atasema, Kuna machinjo katika watu wanaofuatana na Absalomu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata sasa amekwisha kujificha katika pango moja au nafasi ingine. Ikiwa tu katika mashambulizi ya mwanzo kunakufa watu kati yetu, habari itasambaa kwamba wafuasi wa Abusaloma wameshindwa vibaya.