2 Samuel 18:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini yule mtu akamwambia Yoabu, “Hata kama ningeuona uzito wa vipande 1,000 vya fedha mkononi mwangu, nisingeunyosha mkono wangu dhidi ya mwana wa mfalme. Maana, tulimsikia mfalme alipokuamuru wewe Abishai na Itai kwamba, kwa ajili yake, mumlinde kijana Absalomu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini huyo mtu akamjibu Yoabu, “Hata kama ningepimiwa shekeli elfu moja mikononi mwangu, nisingeinua mkono wangu dhidi ya mwana wa mfalme. Tukiwa tunasikia, mfalme alikuagiza wewe na Abishai pamoja na Itai, akisema, ‘Mlindeni kijana Absalomu kwa ajili yangu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule mtu akamwambia Yoabu, Kama ningalipata fedha elfu mkononi mwangu, hata hivyo singalinyosha mkono wangu juu ya mwana wa mfalme; kwa maana mfalme masikioni mwetu alikuagiza wewe, na Abishai na Itai, akisema, Angalieni sana mtu awaye yote asimguse yule kijana, Absalomu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini yule mtu akamwambia Yoabu, “Hata kama ningeuona uzito wa vipande 1,000 vya fedha mkononi mwangu, nisingeunyosha mkono wangu dhidi ya mwana wa mfalme. Maana, tulimsikia mfalme alipokuamuru wewe Abishai na Itai kwamba, kwa ajili yake, mumlinde kijana Absalomu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini huyo mtu akajibu, “Hata kama ningepimiwa shekeli 1,000 mikononi mwangu, nisingeinua mkono wangu dhidi ya mwana wa mfalme. Tukiwa tunasikia, mfalme alikuagiza wewe na Abishai pamoja na Itai, akisema, ‘Mlindeni kijana Absalomu kwa ajili yangu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini huyo mtu akamjibu Yoabu, “Hata kama ningepimiwa shekeli 1,000 mikononi mwangu, nisingeinua mkono wangu dhidi ya mwana wa mfalme. Tukiwa tunasikia, mfalme alikuagiza wewe na Abishai pamoja na Itai, akisema, ‘Mlindeni kijana Absalomu kwa ajili yangu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yule mtu akamwambia Yoabu, Kama ningalipata fedha elfu moja mkononi mwangu, hata hivyo singalinyosha mkono wangu juu ya mwana wa mfalme; kwa maana mfalme masikioni mwetu alikuagiza wewe, na Abishai na Itai, akisema, Angalieni sana mtu yeyote yule asimguse yule kijana, Absalomu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini yule mtu akamwambia Yoabu, “Hata kama ningeuona uzito wa vipande 1,000 vya fedha mkononi mwangu, nisingeunyosha mkono wangu dhidi ya mwana wa mfalme. Maana, tulimsikia mfalme alipokuamuru wewe Abishai na Itai kwamba, kwa ajili yake, mumlinde kijana Absalomu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule mtu akamwambia Yoabu: Ijapo ningepimiwa mimi fedha elfu mikononi mwangu, nisingemkunjulia mwana wa mfalme mkono wa kumpiga, kwani masikioni petu mfalme amekuagiza wewe na Abisai na Itai kwamba: Niangalieni mvulana Abisalomu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule mtu akamwambia Yoabu, Kama ningalipata fedha elfu mkononi mwangu, hata hivyo singalinyosha mkono wangu juu ya mwana wa mfalme; kwa maana mfalme masikioni mwetu alikuagiza wewe, na Abishai na Itai, akisema, Angalieni sana mtu awaye yote asimguse yule kijana, Absalomu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini yule mutu akamwambia Yoabu: “Hata kama ningeuona uzito wa vikoroti elfu moja vya feza katika mukono wangu, singeunyoosha mukono wangu juu ya mwana wa mufalme kwa kumwua. Maana, tulimusikia mufalme alipokuamuru wewe Abisayi na Itayi, kwamba kwa ajili yake, mumulinde kijana Abusaloma.