2 Samuel 18:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoabu akamwambia, “Mimi sina wakati wa kupoteza pamoja nawe.” Hapo Yoabu akachukua mikuki midogo mitatu mkononi mwake, akaenda na kumchoma Absalomu moyoni, Absalomu akiwa bado hai kwenye tawi la mwaloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yoabu akasema, “Mimi sitapoteza muda hapa pamoja nawe.” Hivyo akachukua mikuki mitatu mkononi mwake, akamchoma Absalomu nayo moyoni alipokuwa angali hai akining’inia katika ule mwaloni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Yoabu akasema, Siwezi kungoja na kusema nawe hivi. Akachukua vyemba vitatu mkononi mwake, akamchoma Absalomu moyoni, alipokuwa akali hai katikati ya ule mwaloni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoabu akamwambia, “Mimi sina wakati wa kupoteza pamoja nawe.” Hapo Yoabu akachukua mikuki midogo mitatu mkononi mwake, akaenda na kumchoma Absalomu moyoni, Absalomu akiwa bado hai kwenye tawi la mwaloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yoabu akasema, “Mimi sitapoteza muda hapa pamoja nawe.” Hivyo akachukua mikuki mitatu mkononi mwake na kumchoma nayo Absalomu kwenye moyo alipokuwa angali hai akiwa ananing'inia katika ule mwaloni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yoabu akasema, “Mimi sitapoteza muda hapa pamoja nawe.” Hivyo akachukua mikuki mitatu mkononi mwake, akamchoma Absalomu nayo moyoni alipokuwa angali hai akining’inia katika ule mwaloni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Yoabu akasema, Siwezi kungoja na kusema nawe hivi. Akachukua mikuki mitatu midogo mkononi mwake, akamchoma Absalomu moyoni, alipokuwa bado hai katikati ya ule mwaloni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoabu akamwambia, “Mimi sina wakati wa kupoteza pamoja nawe.” Hapo Yoabu akachukua mikuki midogo mitatu mkononi mwake, akaenda na kumchoma Absalomu moyoni, Absalomu akiwa bado hai kwenye tawi la mwaloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yoabu akasema: Haifai, nikijikawilisha huku kwako. Akachukua mikuki mitatu mkononi mwake, akamchoma nayo Abisalomu moyoni, angaliko mzima mlemle mkwajuni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Yoabu akasema, Siwezi kungoja na kusema nawe hivi. Akachukua vyemba vitatu mkononi mwake, akamchoma Absalomu moyoni, alipokuwa akali hai katikati ya ule mwaloni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoabu akamwambia: “Mimi sina wakati wa kupoteza pamoja nawe.” Yoabu akatwaa mikuki midogo mitatu katika mukono wake, akaenda na kumuchoma Abusaloma ndani ya moyo, Abusaloma akiwa angali muzima kwenye tawi la muti wa mwalo.