2 Samuel 18:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamchukua Absalomu wakamtupa kwenye shimo kubwa msituni na kurundika rundo kubwa sana la mawe. Watu wote wa Israeli wakakimbia, kila mmoja nyumbani kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamchukua Absalomu, wakamtupa katika shimo kubwa huko msituni na kulundika lundo kubwa la mawe juu yake. Huko nyuma, Waisraeli wote wakakimbilia nyumbani mwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakamtwaa Absalomu wakamtupa katika shimo kubwa mle msituni, wakaweka juu yake chungu kubwa sana la mawe; kisha Israeli wote wakakimbia kila mtu hemani mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamchukua Absalomu wakamtupa kwenye shimo kubwa msituni na kurundika rundo kubwa sana la mawe. Watu wote wa Israeli wakakimbia, kila mmoja nyumbani kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamchukua Absalomu, wakamtupa katika shimo kubwa huko msituni na kulundika lundo kubwa la mawe juu yake. Huko nyuma, Waisraeli wote wakakimbilia nyumbani kwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamchukua Absalomu, wakamtupa katika shimo kubwa huko msituni na kulundika lundo kubwa la mawe juu yake. Huko nyuma, Waisraeli wote wakakimbilia nyumbani kwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakamtwaa Absalomu wakamtupa katika shimo kubwa mle msituni, wakaweka juu yake rundo kubwa sana la mawe; kisha Israeli wote wakakimbia kila mtu hemani mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakamchukua Absalomu wakamtupa kwenye shimo kubwa msituni na kurundika rundo kubwa sana la mawe. Watu wote wa Israeli wakakimbia, kila mmoja nyumbani kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamchukua Abisalomu, wakamtupa mle mwituni katika shimo kubwa, juu yake wakakusanya mawe kuwa chungu kubwa sana. Kisha Waisiraeli wote wakakimbilia kila mtu hemani kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakamtwaa Absalomu wakamtupa katika shimo kubwa mle msituni, wakaweka juu yake chungu kubwa sana la mawe; kisha Israeli wote wakakimbia kila mtu hemani mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamukamata Abusaloma, wakamutupia ndani ya shimo kubwa katika pori na kulundika lundo kubwa sana la mawe juu yake. Watu wote wa Israeli wakakimbia, kila mumoja kwake.