2 Samuel 18:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Ahimaasi akamwambia mfalme kwa sauti kubwa, “Mambo yote ni sawa.” Akainama mbele ya mfalme, akasujudu na kusema, “Na atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ambaye amekukomboa kutoka watu walioinua mikono yao dhidi yako, bwana wangu mfalme.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Ahimaasi akamwita mfalme, akasema, “Mambo yote ni mema!” Akasujudu mbele ya mfalme, uso wake ukigusa chini, akasema, “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wako! Yeye aliyewatoa watu wale walioinua mikono yao dhidi ya mfalme bwana wangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ahimaasi akainua sauti yake, akamwambia mfalme, Amani. Akainama mbele ya mfalme kifudifudi, akasema, Ahimidiwe Bwana, Mungu wako, aliyewatoa watu hao walioiinua mikono yao juu ya bwana wangu, mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Ahimaasi akamwambia mfalme kwa sauti kubwa, “Mambo yote ni sawa.” Akainama mbele ya mfalme, akasujudu na kusema, “Na atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ambaye amekukomboa kutoka watu walioinua mikono yao dhidi yako, bwana wangu mfalme.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Ahimaasi akamwita mfalme, akasema, “Mambo yote ni mema!” Akasujudu mbele ya mfalme uso wake mpaka ardhini, akasema, “Ahimidiwe BWANA Mungu wako! Yeye aliyewatoa watu wale walioinua mikono yao dhidi ya mfalme bwana wangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Ahimaasi akamwita mfalme, akasema, “Mambo yote ni mema!” Akasujudu mbele ya mfalme uso wake mpaka ardhini, akasema, “Ahimidiwe bwana Mwenyezi Mungu wako! Yeye aliyewatoa watu wale walioinua mikono yao dhidi ya mfalme bwana wangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ahimaasi akainua sauti yake, akamwambia mfalme, Amani. Akainama mbele ya mfalme kifudifudi, akasema, Ahimidiwe BWANA, Mungu wako, aliyewatoa watu hao walioiinua mikono yao juu ya bwana wangu, mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Ahimaasi akamwambia mfalme kwa sauti kubwa, “Mambo yote ni sawa.” Akainama mbele ya mfalme, akasujudu na kusema, “Na atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ambaye amekukomboa kutoka watu walioinua mikono yao dhidi yako, bwana wangu mfalme.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ahimasi akaita na kumwambia mfalme: Pongezi! Kisha akamwangukia mfalme na kujiangusha chini kifudifudi, akasema: Bwana Mungu wako na atukuzwe! Kwani wao waliomwinulia bwana wangu mfalme mikono yao amewatoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ahimaasi akainua sauti yake, akamwambia mfalme, Amani. Akainama mbele ya mfalme kifudifudi, akasema, Ahimidiwe BWANA, Mungu wako, aliyewatoa watu hao walioiinua mikono yao juu ya bwana wangu, mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Ahimasi akamwambia mufalme kwa sauti kubwa: “Mambo yote ni sawa.” Akainama mbele ya mufalme, kwa heshima na kusema: “Yawe atukuzwe, Mungu wako, ambaye amekukomboa kutoka watu walioinua mikono yao juu yako, bwana wangu mufalme.”