2 Samuel 18:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo na yule Mkushi akafika; naye akasema, “Kuna habari njema kwako bwana wangu mfalme! Maana Mwenyezi-Mungu leo hii amekukomboa kutoka nguvu za wale wote walioinuka dhidi yako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo huyo Mkushi akawasili na kusema, “Mfalme bwana wangu, sikia habari njema! Leo Mwenyezi Mungu amekuokoa kutoka kwa wale wote walioinuka dhidi yako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, yule Mkushi akafika; Mkushi akasema, Nina habari kwa bwana wangu mfalme; kwa maana Bwana amekulipizia kisasi leo juu ya hao wote walioinuka kupigana nawe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo na yule Mkushi akafika; naye akasema, “Kuna habari njema kwako bwana wangu mfalme! Maana Mwenyezi-Mungu leo hii amekukomboa kutoka nguvu za wale wote walioinuka dhidi yako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo huyo Mkushi akawasili na kusema, “Mfalme bwana wangu, sikia habari njema! Leo BWANA amekuokoa kutoka kwa wale wote walioinuka dhidi yako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo huyo Mkushi akawasili na kusema, “Mfalme bwana wangu, sikia habari njema! Leo bwana amekuokoa kutoka kwa wale wote walioinuka dhidi yako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, yule Mkushi akafika; Mkushi akasema, Nina habari kwa bwana wangu mfalme; kwa maana BWANA amekulipizia kisasi leo juu ya hao wote walioinuka kupigana nawe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo na yule Mkushi akafika; naye akasema, “Kuna habari njema kwako bwana wangu mfalme! Maana Mwenyezi-Mungu leo hii amekukomboa kutoka nguvu za wale wote walioinuka dhidi yako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara yule Mnubi akaja, naye akasema kwamba: Bwana wangu mfalme na ausikie huu utume mwema, ya kuwa Bwana amekuamulia leo na kukuokoa mikononi mwao wote waliokuinukia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, yule Mkushi akafika; Mkushi akasema, Nina habari kwa bwana wangu mfalme; kwa maana BWANA amekulipizia kisasi leo juu ya hao wote walioinuka kupigana nawe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu yule Mwetiopia akafika; naye akasema: “Kuna habari njema kwako bwana wangu mufalme! Maana Yawe leo hii amekukomboa kutoka nguvu za wale wote waliokushambulia.”