2 Samuel 18:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme akamwuliza, “Je kijana Absalomu hajambo?” Mkushi akasema, “Maadui wako, bwana wangu mfalme, pamoja na wote wanaoinuka dhidi yako wakikutakia mabaya, wawe kama huyo kijana Absalomu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akamuuliza huyo Mkushi, “Je, kijana Absalomu yuko salama?” Huyo Mkushi akajibu, “Adui wa mfalme bwana wangu na wote wale walioinuka kukudhuru na wawe kama huyo kijana.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye mfalme akamwambia yule Mkushi, Yule kijana, Absalomu, je! Yu salama? Yule Mkushi akajibu, Adui za bwana wangu mfalme, na wote wainukao ili kukudhuru, na wawe kama alivyo yule kijana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme akamwuliza, “Je kijana Absalomu hajambo?” Mkushi akasema, “Maadui wako, bwana wangu mfalme, pamoja na wote wanaoinuka dhidi yako wakikutakia mabaya, wawe kama huyo kijana Absalomu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akamwuliza huyo Mkushi, “Je, kijana Absalomu yuko salama?” Huyo Mkushi akajibu, “Adui wa mfalme bwana wangu na wote wale walioinuka kukudhuru na wawe kama huyo kijana.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akamuuliza huyo Mkushi, “Je, kijana Absalomu yuko salama?” Huyo Mkushi akajibu, “Adui wa mfalme bwana wangu na wote wale walioinuka kukudhuru na wawe kama huyo kijana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye mfalme akamwambia yule Mkushi, Yule kijana, Absalomu, je! Yuko salama? Yule Mkushi akajibu, Adui za bwana wangu mfalme, na wote wainukao ili kukudhuru, na wawe kama alivyo yule kijana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme akamwuliza, “Je kijana Absalomu hajambo?” Mkushi akasema, “Maadui wako, bwana wangu mfalme, pamoja na wote wanaoinuka dhidi yako wakikutakia mabaya, wawe kama huyo kijana Absalomu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akamwuliza huyu Mnubi naye: Mvulana Abisalomu hajambo? Huyu Mnubi akasema: Adui wote wa mfalme na wafanyiziwe kama huyo mvulana! Nao wote waliokuinukia kufanya mabaya na wawe hivyo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye mfalme akamwambia yule Mkushi, Yule kijana, Absalomu, je! Yu salama? Yule Mkushi akajibu, Adui za bwana wangu mfalme, na wote wainukao ili kukudhuru, na wawe kama alivyo yule kijana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akamwuliza: “Kijana Abusaloma ni muzima?” Mwetiopia akasema: “Waadui zako, bwana wangu mufalme, pamoja na wote wanaokushambulia wakikutakia mabaya, wakuwe kama huyo kijana Abusaloma.”