2 Samuel 18:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme akawaambia, “Lolote mnaloona ni bora kwenu, nitalitenda.” Hivyo, mfalme akasimama kando ya lango, huku jeshi lake likipita: Mamia na maelfu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akajibu, “Nitafanya lolote linaloonekana jema zaidi kwenu.” Kwa hiyo mfalme akasimama kando ya lango wakati watu wote wakitoka nje kwa makundi ya mamia na maelfu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akawaambia, Yaliyo mema machoni penu ndiyo nitakayofanya. Basi mfalme akasimama kando ya lango, na hao watu wakatoka kwa elfu zao na mia zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme akawaambia, “Lolote mnaloona ni bora kwenu, nitalitenda.” Hivyo, mfalme akasimama kando ya lango, huku jeshi lake likipita: mamia na maelfu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akajibu, “Nitafanya lo lote linaloonekana jema zaidi kwenu.” Kwa hiyo mfalme akasimama kando ya lango wakati watu wote wakitoka nje kwa makundi ya mamia na maelfu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akajibu, “Nitafanya lolote linaloonekana jema zaidi kwenu.” Kwa hiyo mfalme akasimama kando ya lango wakati watu wote wakitoka nje kwa makundi ya mamia na maelfu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme akawaambia, Yaliyo mema machoni penu ndiyo nitakayofanya. Basi mfalme akasimama kando ya lango, na hao watu wakatoka kwa maeelfu yao na mamia yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme akawaambia, “Lolote mnaloona ni bora kwenu, nitalitenda.” Hivyo, mfalme akasimama kando ya lango, huku jeshi lake likipita: Mamia na maelfu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akawaitikia kwamba: Yaliyo mema machoni penu, basi, nitayafanya. Kisha mfalme akaja kusimama kando penye lango la mji, nao watu wote wakatoka mia kwa mia, na elfu kwa elfu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akawaambia, Yaliyo mema machoni penu ndiyo nitakayofanya. Basi mfalme akasimama kando ya lango, na hao watu wakatoka kwa elfu zao na mia zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akawaambia: “Nitafanya sawa vile munavyoona kuwa vizuri.” Kwa hiyo, mufalme akasimama pembeni ya mulango, nao waaskari wake wakipita: mamia na maelfu.