2 Samuel 18:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme akawaamuru Yoabu, Abishai na Itai, “Kwa ajili yangu, mtendeeni yule kijana Absalomu kwa upole.” Watu wote walimsikia mfalme alipoamuru makamanda wake kuhusu Absalomu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akawaamuru Yoabu, Abishai na Itai, “Kuweni wapole kwa kijana Absalomu kwa ajili yangu.” Vikosi vyote vikasikia mfalme akitoa amri kwa kila jemadari kumhusu Absalomu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akawaamuru Yoabu na Abishai na Itai, akasema, Mtendeeni yule kijana, Absalomu, kwa upole kwa ajili yangu. Nao watu wote wakasikia, mfalme alipowaagiza maakida wote katika habari za Absalomu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme akawaamuru Yoabu, Abishai na Itai, “Kwa ajili yangu, mtendeeni yule kijana Absalomu kwa upole.” Watu wote walimsikia mfalme alipoamuru makamanda wake kuhusu Absalomu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akawaamuru Yoabu, Abishai na Itai, “Iweni wapole kwa kijana Absalomu kwa ajili yangu.” Vikosi vyote vikasikia mfalme akitoa amri kwa kila jemadari kumhusu Absalomu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akawaamuru Yoabu, Abishai na Itai, “Kuweni wapole kwa kijana Absalomu kwa ajili yangu.” Vikosi vyote vikasikia mfalme akitoa amri kwa kila jemadari kumhusu Absalomu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme akawaamuru Yoabu na Abishai na Itai, akasema, Mtendeeni yule kijana, Absalomu, kwa upole kwa ajili yangu. Nao watu wote wakasikia, mfalme alipowaagiza makamanda wote kuhusu Absalomu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme akawaamuru Yoabu, Abishai na Itai, “Kwa ajili yangu, mtendeeni yule kijana Absalomu kwa upole.” Watu wote walimsikia mfalme alipoamuru makamanda wake kuhusu Absalomu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipomwagiza Yoabu na Abisai na Itai wa Gati kwamba: Nataka hili tu, mmwendee mvulana Abisalomu kwa upole! watu wote wakayasikia, mfalme alipowaagiza wakuu wote hayo kwa ajili ya Abisalomu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akawaamuru Yoabu na Abishai na Itai, akasema, Mtendeeni yule kijana, Absalomu, kwa upole kwa ajili yangu. Nao watu wote wakasikia, mfalme alipowaagiza maakida wote katika habari za Absalomu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akawaamuru Yoabu, Abisayi na Itayi: “Kwa ajili yangu, mumutendee yule kijana Abusaloma kwa upole.” Watu wote walimusikia mufalme alipoamuru wakubwa wake juu ya Abusaloma.