2 Samuel 18:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Absalomu, akiwa amepanda nyumbu, alikutana na watumishi wa Daudi. Nyumbu huyo alipokuwa anapita chini ya tawi kubwa la mwaloni, hapo kichwa cha Absalomu kikakwama kwenye mwaloni. Absalomu akaachwa ananinginia juu. Lakini nyumbu wake akaendelea mbele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi ikawa Absalomu alikutana na watu wa Daudi. Yeye alikuwa amepanda nyumbu wake, naye nyumbu alipopita chini ya matawi yaliyosongamana ya mwaloni mkubwa, kichwa cha Absalomu kilinaswa kwenye mti. Akaachwa akining’inia hewani, wakati nyumbu aliyekuwa amempanda aliendelea kwenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa bahati Absalomu akakutana na watumishi wa Daudi. Naye Absalomu alikuwa amepanda nyumbu wake, na yule nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa, hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo, akanyakuliwa juu kati ya mbingu na nchi; na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Absalomu, akiwa amepanda nyumbu, alikutana na watumishi wa Daudi. Nyumbu huyo alipokuwa anapita chini ya tawi kubwa la mwaloni, hapo kichwa cha Absalomu kikakwama kwenye mwaloni. Absalomu akaachwa ananing'inia juu. Lakini nyumbu wake akaendelea mbele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi ikawa Absalomu alikutana na watu wa Daudi. Yeye alikuwa amepanda nyumbu wake, naye nyumbu alipopita chini ya matawi yaliyosongana ya mwaloni mkubwa, kichwa cha Absalomu kilinaswa kwenye mti. Akaachwa ananing'inia hewani, wakati nyumbu aliyekuwa amempanda aliendelea kwenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi ikawa Absalomu alikutana na watu wa Daudi. Yeye alikuwa amepanda nyumbu wake, naye nyumbu alipopita chini ya matawi yaliyosongana ya mwaloni mkubwa, kichwa cha Absalomu kilinaswa kwenye mti. Akaachwa akining’inia hewani, wakati nyumbu aliyekuwa amempanda aliendelea kwenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kwa bahati Absalomu akakutana na watumishi wa Daudi. Naye Absalomu alikuwa amepanda nyumbu wake, na yule nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa, hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo, akanyakuliwa juu kati ya mbingu na nchi; na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Absalomu, akiwa amepanda nyumbu, alikutana na watumishi wa Daudi. Nyumbu huyo alipokuwa anapita chini ya tawi kubwa la mwaloni, hapo kichwa cha Absalomu kikakwama kwenye mwaloni. Absalomu akaachwa ananinginia juu. Lakini nyumbu wake akaendelea mbele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikatukia, watumishi wa Dawidi wamwone Abisalomu, naye Abisalomu alikuwa amepanda nyumbu; huyo nyumbu alipopita chini ya mkwaju mkubwa wenye matawi mengi yaliyofungamana, mara tawi moja likakikamata kichwa chake mlemle katika mkwaju, hivyo akaangikwa katikati ya mbingu na nchi, kwani nyumbu aliyekuwa chini yake alikimbia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa bahati Absalomu akakutana na watumishi wa Daudi. Naye Absalomu alikuwa amepanda nyumbu wake, na yule nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa, hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo, akanyakuliwa juu kati ya mbingu na nchi; na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Abusaloma, akiwa amepanda juu ya nyumbu, alikutana na watumishi wa Daudi. Nyumbu huyo alipokuwa anapita chini ya tawi kubwa la muti wa mwalo, halafu kichwa cha Abusaloma kikakwama kwenye muti wa mwalo. Abusaloma akaachwa akilembelea katika hewa. Lakini nyumbu wake akaendelea mbele.