2 Samuel 19:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwulizeni pia Amasa kama yeye si damu yangu. Tena Mungu aniue ikiwa simfanyi yeye kuwa kamanda wa jeshi langu tangu leo badala ya Yoabu.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi mwambieni Amasa, ‘Je, wewe si mwili wangu mwenyewe na damu yangu? Mungu na aniadhibu vikali zaidi, kama kuanzia sasa na kuendelea wewe si jemadari wa jeshi langu mahali pa Yoabu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha mkamwambie Amasa, Je! Si wewe uliye mfupa wangu, na nyama yangu? Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, usipokuwa wewe jemadari wa jeshi mbele yangu daima mahali pa Yoabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwulizeni pia Amasa kama yeye si damu yangu. Tena Mungu aniue ikiwa simfanyi yeye kuwa kamanda wa jeshi langu tangu leo badala ya Yoabu.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi mwambieni Amasa, ‘Je, wewe si nyama yangu mwenyewe na damu yangu? Mungu na anishughulikie, tena kwa ukali, kama kuanzia sasa na kuendelea wewe si jemadari wa jeshi langu mahali pa Yoabu.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi mwambieni Amasa, ‘Je, wewe si nyama yangu mwenyewe na damu yangu? Mungu na anishughulikie, tena kwa ukali, kama kuanzia sasa na kuendelea wewe si jemadari wa jeshi langu mahali pa Yoabu.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha mkamwambie Amasa, Je! Si wewe uliye mfupa wangu, na nyama yangu? Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, usipokuwa wewe jemadari wa jeshi mbele yangu daima mahali pa Yoabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwulizeni pia Amasa kama yeye si damu yangu. Tena Mungu aniue ikiwa simfanyi yeye kuwa kamanda wa jeshi langu tangu leo badala ya Yoabu.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Amasa mwambieni: Kumbe wewe na mimi mifupa yetu siyo ya mmoja, nazo nyama za miili yetu sizo za mmoja? Mungu na anifanyizie hivi na hivi, wewe usipopata kwangu kuwa mkuu wa vikosi siku zote mahali pake Yoabu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha mkamwambie Amasa, Je! Si wewe uliye mfupa wangu, na nyama yangu? Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, usipokuwa wewe jemadari wa jeshi mbele yangu daima mahali pa Yoabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi ni wandugu zangu, ninyi ni damu yangu. Kwa nini mukuwe wa mwisho kunirudisha mimi mufalme kwangu?